Asidi ya 4-Aminosalicylic
Asidi ya 4-Aminosalicylic, pia inajulikana kama asidi ya para -aminosalicylic (PAS) na kuuzwa chini ya jina la chapa la Paser miongoni mwa mengineyo, ni dawa inayotumika kutibu kifua kikuu.[1] Hasa hutumika kutibu kifua kikuu sugu kwa dawa pamoja na dawa zingine za kuzuia kifua kikuu.[2] Pia imetumika kama wakala wa safu ya pili wa sulfasalazine kwa watu walio na ugonjwa wa uvimbe wa matumbo kama vile ugonjwa wa ulcerative na ugonjwa wa Crohn.[2] Kwa kawaida inachukuliwa kwa mdomo.[2]
Jina la Utaratibu la (IUPAC) | |
---|---|
4-Amino-2-hydroxybenzoic acid | |
Data ya kikliniki | |
Majina ya kibiashara | Paser, Granupas, na mengineyo |
AHFS/Drugs.com | Monograph |
Taarifa za leseni | US Daily Med:link |
Kategoria ya ujauzito | C(US) |
Hali ya kisheria | ℞-only (US) ℞ Prescription only |
Njia mbalimbali za matumizi | Kwa mdomo |
Data ya utendakazi | |
Kufunga kwa protini | 50–60% |
Kimetaboliki | Ini |
Utoaji wa uchafu | Figo |
Vitambulisho | |
Nambari ya ATC | ? |
Data ya kikemikali | |
Fomyula | C7H7NO3 |
| |
Data ya kimwili | |
Kiwango cha kuyeyuka | 150.5 °C (303 °F) |
(Hiki ni nini?) (thibitisha) |
Madhara yake ya kawaida ni pamoja na kichefuchefu, maumivu ya tumbo na kuhara.[2] Madhara yake mengine yanaweza kujumuisha kuvimba kwa ini na athari za mzio.[2] Haipendekezwi kwa watu walio na ugonjwa wa figo wa hatua ya mwisho.[2] Ingawa matumizi yake hayaonekani kuwa na madhara wakati wa ujauzito, haijafanyiwa utafiti vizuri katika suala hili.[2] Asidi ya 4-Aminosalicylic inaaminika kufanya kazi kwa kuzuia uwezo wa bakteria kutengeneza asidi ya foliki (folic acid).[2]
Asidi ya 4-Aminosalicylic ilitengenezwa kwa mara ya kwanza mwaka wa 1902, na ilianza kutumika katika matibabu mwaka wa 1943.[3] Iko kwenye Orodha ya Dawa Muhimu ya Shirika la Afya Ulimwenguni.[4] As of 2005[update] Kufikia mwaka wa 2005, matibabu ya kifua kikuu yamegharimu takriban dola za Marekani 2,700.[5]
Marejeleo
hariri- ↑ World Health Organization (2009). Stuart MC, Kouimtzi M, Hill SR (whr.). WHO Model Formulary 2008. World Health Organization. uk. 140. hdl:10665/44053. ISBN 9789241547659.
- ↑ 2.0 2.1 2.2 2.3 2.4 2.5 2.6 2.7 "Aminosalicylic Acid". The American Society of Health-System Pharmacists. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 20 Desemba 2016. Iliwekwa mnamo 8 Desemba 2016.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ Donald PR, Diacon AH (Septemba 2015). "Para-aminosalicylic acid: the return of an old friend". Lancet Infectious Diseases. 15 (9): 1091–99. doi:10.1016/s1473-3099(15)00263-7. PMID 26277036.
{{cite journal}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ World Health Organization (2019). World Health Organization model list of essential medicines: 21st list 2019. Geneva: World Health Organization. hdl:10665/325771. WHO/MVP/EMP/IAU/2019.06. License: CC BY-NC-SA 3.0 IGO.
- ↑ Brown, Garrett W.; Yamey, Gavin; Wamala, Sarah (2014-04-08). "Chapter 12". The Handbook of Global Health Policy. John Wiley & Sons. ISBN 9781118509609. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2016-12-20.