Ugonjwa wa vidonda vya utumbo mkubwa
Ugonjwa wa vidonda vya utumbo mkubwa (kwa Kiingereza: Ulcerative colitis, kifupi: UC) ni hali ya muda mrefu ambayo husababisha kuvimba na vidonda kwenye utumbo mkubwa na rektamu.[1][5] Dalili kuu za ugonjwa uliopo ni maumivu ya tumbo na kuhara kulikochanganyika na damu.[1] Kupungua kwa uzani, homa, na anemia pia ni dalili.[1] Mara nyingi, dalili huanza polepole na zinaweza kuwa kati ya ndogo hadi kali.[1] Dalili hujitokeza mara kwa mara na vipindi vya kutokuwepo kwa dalili kati ya milipuko ya dalili.[1] Matatizo yanaweza kujumuisha kupanuka kwa utumbo mkubwa, kuvimba kwa jicho, viungo au ini na saratani ya utumbo mkubwa.[1][6]
Ugonjwa wa vidonda vya utumbo mkubwa | |
---|---|
Mwainisho na taarifa za nje | |
Kundi Maalumu | Gastroenterology |
Dalili | Maumivu ya tumbo, kuhara kulikochanganyika na damu, kupungua kwa uzani, homa, upungufu wa damu[1] |
Muda wa kawaida wa kuanza kwake | Kuanzia miaka 15–30 au > ya umri wa miaka 60[1] |
Muda | Ya muda mrefu[1] |
Visababishi | Havijulikani[1] |
Njia ya kuitambua hali hii | kolonoskopia pamija na biopsi ya tishu[1] |
Utambuzi tofauti | Ugonjwa wa kuhara (Dysentery), Ugonjwa wa Crohn, uvimbe wa utumbo mpana kutokana na ukosefu wa mtiririko wa damu wa kutosha (ischemic colitis)[2] |
Matibabu | Kubadilisha lishe, utumiaji wa dawa, upasuaji[1] |
Dawa | Sulfasalazine, mesalazine, steroidi, dawa zinazozuia utendaji wa mfumo wa kinga kama vile azathioprine, tiba ya kibiolojia[1] |
Idadi ya utokeaji wake | Hadi watu 5 kwa kila watu 1000[3] |
Vifo | watu 47,400 pamoja na ugonjwa wa Crohn (2015)[4] |
Kisababishi cha UC hakijulikani.[1] Nadharia zinahusisha kutofanya kazi kwa mfumo wa kinga, jeni, mabadiliko ya bakteria za kawaida za utumbo na mambo ya kimazingira.[1][7] Viwango vya ugonjwa huu vinaonekana kuwa vyu juu zaidi kwenye nchi zilizostawi huku wengine wakipendekeza kuwa haya ni matokeo ya kuathiriwa kwa kiwango cha chini na maambukizo ya utumbo au kutokana na lishe na mtindo wa maisha wa mataifa ya Magharibi.[5][8] Kuondolewa kwa kidole cha tumbo katika umri mdogo kunaweza kuwa kinga.[8] Utambuzi kwa kawaida hufanywa kupitia kolonoskopia pamoja na biopsi ya tishu.[1] Ni aina ya ugonjwa wa matumbo unaosababisha kuvimba (IBD) pamoja na ugonjwa wa Crohn na uvimbe mdogo wa utumbo mkubwa.[1]
Mabadiliko ya lishe, kama vile kuendelea kuendelea kula lishe yenye kalori nyingi au lishe isiyo na laktosi, yanaweza kuboresha dalili.[1] Dawa kadhaa hutumiwa kutibu dalili na kusababisha na kudumisha hali ya kupungua kwa dalili, zikiwemo aminosalicylates kama mesalazine au sulfasalazine, steroidi, dawa zinazozuia utendaji wa mfumo wa kinga kama vile azathioprine na tiba ya kibiolojia.[1] Kuondolewa kwa utumbo mkubwa kupitia upasuaji kunaweza kuwa muhimu ikiwa ugonjwa umekithiri, haukubali matibabu au ikiwa matatizo kama vile saratani ya utumbo mkubwa yataibuka.[1] Kuondolewa kwa utumbo mkubwa na rektamu kwa ujumla huponya hali hiyo.[1][8]
Pamoja na ugonjwa wa Crohn, uliathiri takriban watu milioni 11.2 kufikia mwaka wa 2015.[9] Kila mwaka, hujitokeza upya kwa mtu 1 hadi watu 20 kati ya watu 100,000 na watu 5 hadi 500 kati ya watu 100,000 huathiriwa.[5][8] Ugonjwa huu unaripotiwa zaidi katika Amerika ya Kaskazini na Ulaya kuliko maeneo mengine.[8] Mara nyingi huanza kwa watu wenye umri wa miaka 15 hadi 30 au walio na umri wa zaidi ya miaka 60.[1] Wanaume na wanawake wanaonekana kuathiriwa kwa uwiano sawa.[5] Pia umeripotiwa zaidi tangu miaka ya 1950.[5][8] Kwa pamoja, ugonjwa wa uvimbe wa utumbo mkubwa na ugonjwa wa Crohn huathiri watu wapatao milioni moja nchini Marekani.[10] Kwa matibabu yanayofaa, hatari ya kifo inaonekana kuwa sawa na ile ya idadi ya watu kwa ujumla.[6] Maelezo ya kwanza ya ugonjwa wa vidonda vya utumbo mkubwa yalitokea karibia miaka ya 1850.[8]
Marejeo
hariri- ↑ 1.00 1.01 1.02 1.03 1.04 1.05 1.06 1.07 1.08 1.09 1.10 1.11 1.12 1.13 1.14 1.15 1.16 1.17 1.18 1.19 "Ulcerative Colitis". NIDDK. Septemba 2014. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 28 Julai 2016. Iliwekwa mnamo 3 Agosti 2016.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ Runge, Marschall S.; Greganti, M. Andrew (2008). Netter's Internal Medicine E-Book (kwa Kiingereza). Elsevier Health Sciences. uk. 428. ISBN 9781437727722. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 27 Agosti 2021. Iliwekwa mnamo 27 Julai 2020.
{{cite book}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ Molodecky NA, Soon IS, Rabi DM, Ghali WA, Ferris M, Chernoff G, Benchimol EI, Panaccione R, Ghosh S, Barkema HW, Kaplan GG (Januari 2012). "Increasing incidence and prevalence of the inflammatory bowel diseases with time, based on systematic review". Gastroenterology. 142 (1): 46–54.e42, quiz e30. doi:10.1053/j.gastro.2011.10.001. PMID 22001864.
{{cite journal}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ Wang H, Naghavi M, Allen C, Barber RM, Bhutta ZA, Carter A, na wenz. (GBD 2015 Mortality and Causes of Death Collaborators) (Oktoba 2016). "Global, regional, and national life expectancy, all-cause mortality, and cause-specific mortality for 249 causes of death, 1980–2015: a systematic analysis for the Global Burden of Disease Study 2015". Lancet. 388 (10053): 1459–1544. doi:10.1016/s0140-6736(16)31012-1. PMC 5388903. PMID 27733281.
{{cite journal}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ 5.0 5.1 5.2 5.3 5.4 Ford AC, Moayyedi P, Hanauer SB (Februari 2013). "Ulcerative colitis". BMJ. 346: f432. doi:10.1136/bmj.f432. PMID 23386404.
{{cite journal}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ 6.0 6.1 Wanderås MH, Moum BA, Høivik ML, Hovde Ø (Mei 2016). "Predictive factors for a severe clinical course in ulcerative colitis: Results from population-based studies". World Journal of Gastrointestinal Pharmacology and Therapeutics. 7 (2): 235–41. doi:10.4292/wjgpt.v7.i2.235. PMC 4848246. PMID 27158539.
{{cite journal}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) CS1 maint: unflagged free DOI (link) - ↑ Akiho H, Yokoyama A, Abe S, Nakazono Y, Murakami M, Otsuka Y, Fukawa K, Esaki M, Niina Y, Ogino H (Novemba 2015). "Promising biological therapies for ulcerative colitis: A review of the literature". World Journal of Gastrointestinal Pathophysiology. 6 (4): 219–27. doi:10.4291/wjgp.v6.i4.219. PMC 4644886. PMID 26600980.
{{cite journal}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) CS1 maint: unflagged free DOI (link) - ↑ 8.0 8.1 8.2 8.3 8.4 8.5 8.6 Danese S, Fiocchi C (Novemba 2011). "Ulcerative colitis". The New England Journal of Medicine. 365 (18): 1713–25. doi:10.1056/NEJMra1102942. PMID 22047562.
{{cite journal}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ Vos T, Allen C, Arora M, Barber RM, Bhutta ZA, Brown A, na wenz. (Oktoba 2016). "Global, regional, and national incidence, prevalence, and years lived with disability for 310 diseases and injuries, 1990–2015: a systematic analysis for the Global Burden of Disease Study 2015". Lancet. 388 (10053): 1545–1602. doi:10.1016/S0140-6736(16)31678-6. PMC 5055577. PMID 27733282.
{{cite journal}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ Adams, James G. (2012). Emergency Medicine E-Book: Clinical Essentials (Expert Consult – Online) (kwa Kiingereza). Elsevier Health Sciences. uk. 304. ISBN 978-1455733941. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 16 Machi 2020. Iliwekwa mnamo 27 Julai 2020.