Astrosaiti ni seli zenye umbo la nyota katika ubongo na mithili ya kamba kwenye uti wa mgongo. Pia hizi seli zinajulikana kwa pamoja kama astroglia.

Astrosaiti
Astrosaiti.

Uwiano wa astrosaiti katika ubongo hutofautiana. Uchunguzi umegundua kuwa uwiano wa astrosaiti hutofautiana na eneo kutoka 20% hadi 40% ya glia zote.

Astrosaiti hufanya mambo mengi: husaidia seli za mwisho za ubongo, hutoa virutubisho kwa tishu za neva, kuweka ioni za ziada kwa usawa. Pia husaidia kurekebisha ubongo na nyuzinyuzi za uti wa mgongo baada ya majeraha.

Makala hii kuhusu mambo ya anatomia bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Astrosaiti kama matumizi yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.