Asilimia

(Elekezwa kutoka %)

Asilimia (kutoka maneno mawili ya Kiarabu اصل asl yaani asili, chanzo na مئوية mia 100 ) ni njia ya kutaja uhusiano kati ya idadi mbili tofauti. Alama yake ni %. Kiasi kimoja huteuliwa kuwa ni namba ya 100 ya kiasi kingine. Sehemu yake ya mia ni 1 %.

Katika ramani (Kulia) ni asilimia ya Watumwa kati ya wakazi wote katika Bara la Marekani, 1860

Sasa inawezekana kugawa kiasi kingine kwa ile 1% na kuona inashika asilimia ngapi za kiasi husianifu.

Mfano hariri

Mfano: Jumla ya maksi kwenye mtihani ni 250. Sheria inasema ya kwamba 65 % ni sharti kwa kupita. Je, maksi ngapi zinahitajika ila kupita mtihani huu?

Jibu: Jumla ni 250, hivyo 250 zachukuliwa kama asilimia mia moja. Sehemu ya mia moja yaani 1 % ni 2.5. Asilimia 65 ni 2.5, zidisha 65 jumla 162.5. Maana yake kuanzia maksi zisizopungua 163 mwanafunzi amepita.

Sehemu na asilimia hariri

Kuna viwango kadhaa za sehemu zinazokumbukwa kirahisi kwa asilimia:

Sehemu Asilimia
Nusu 50 %
robo 25 %
robo tatu 75 %
theluthi 33 %
humusi 20 %
humusi mbili 40 %
ya kumi 10 %


Sehemu kama sudusi haifai vizuri kwa sababu asilimia yake ni 16.66 %.

  Makala hii kuhusu mambo ya hisabati bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Asilimia kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.