Athuman Kabongo (aka Mwanachemba; anafahamika zaidi kwa jina lake la kisanii kama Dark Master) ni msanii wa muziki wa Hip hop, Ragga Dancehall na Bongo flava kutoka nchini Tanzania.

Dark Master Mwanachemba
Jina la kuzaliwa Athuman Kabongo
Pia anajulikana kama Darkmaster Mwanachemba
Amezaliwa 6th Oct 1980
Asili yake Mpare
Aina ya muziki Hip hop/ Dance hall
Kazi yake Hip-hop Mc, Muigizaji
Ala Hip-hop & Ragga Dancehall
Aina ya sauti Bass
Miaka ya kazi 23 yrs
Studio Bongo Records, FM Studio, Backyard Record, One Love Efx, Mo Record, ATP studio, MJ Records, KC Records, K Records, Tongwe Records, Kinasa Studios
Ame/Wameshirikiana na Bushoke, Noorah, Brown punch, Twalib, Juma nature, Ngwea, D-knob, Geez Mabovu, Mez B, Chelea Man, JB Jerusalem, Muhogo mchungu, Richard Mtambalike, Fetty Slay & One six

Alikuwa miongoni mwa mastaa mahiri walioibuka mwishoni mwa miaka ya 90 wakati Bongo Hiphop na Rap zilikuwa zikijulikana.

Darkmaster Mwanachemba alijulikana zaidi kupitia kikundi chake cha muziki cha Chemba Squad, akiwa ni muanzilishi kutoka East Zuu, Dodoma, Tanzania.

Dark Master ameshatoa album mbili moja ikiitwa Mjukuu wa Chimwaga (2011) na ya pili East Zuu Republic "Mc Mkomunist 1" (2022)

Darkmaster Mwanachemba pia amefanya nyimbo kadha wa kadha akishirikishana na wasanii tofauti tofauti, ambazo zilifanikiwa kukaa kwa muda mrefu katika chati za redio na runinga mbalimbali Kimataifa.

Baadhi ya Nyimbo hizo ni pamoja na Shega Tu, Sema Darkie|Darkmaster, Nimepamis Home, East Zuu Father, Hip for Life|HipHop for Life, She Gotta Gwan (kashirikishwa na Mangwair) na nyingine nyingi tu zilizofanywa na msanii huyu.

Shukrani kwa rap yake ya ndani, njia yake nyeti ya kutengeneza hiphop na mguso wake wa dhahabu kwa kuandika kila wimbo wake au kama Crew at Chemba squad Kuanzia 1996 ilishika nafasi ya kwanza kwenye chati nchi nzima.

Tayari ameshafanya videos kadhaa na zinaonekana katika TV.

Darkmaster anaamini jamii ndio imempa dhamana ya kutoa Burudani, na hii ndio maana ya msanii.

Makala hii kuhusu mwanamuziki/wanamuziki fulani wa Tanzania bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Athuman Kabongo kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.