Mangwair
Albert Keneth Mangwair (a.k.a Mimi a.k.a Ngwair; 16 Novemba 1982 - 28 Mei 2013) alikuwa msanii wa Hip Hop ya Bongo kutoka mchini Tanzania.
Mangwair | |
---|---|
Mangwai katika Pozi | |
Taarifa za awali | |
Jina la kuzaliwa | Albert Magwair |
Amezaliwa | Mbeya, Tanzania | Novemba 16, 1982
Amekufa | 28 Mei 2013 (umri 30) Johannesburg, Afrika Kusini |
Kazi yake | Rapper |
Miaka ya kazi | 1999–2013 |
Studio | Bongo Records |
Ameshirikiana na | Daz Baba, Jay Moe, Mchizi Mox, Chamber Squad, Noorah, T. I. D., Ferouz, Mwana FA, Chid Benz, Dullah Platinum (Abdallah Mgeleka na Dark Master, Cpwaa, Dully Sykes |
Maisha ya awali
Alizaliwa na jina la Albert Keneth Mangwair mnamo tar. 16 Novemba, 1982, Mbeya, Tanzania. Kiasili, ni mtu wa Ruvuma, yaani, ni Mngoni. Lakini alizaliw mjini Mbeya na akiwa na umri wa miaka 5, familia yake ilihamia mjini Morogoro kikazi na hatimaye kuanza masomo ya msingi hukohuko mjini Morogoro hadi darasa la 5 na kupata uhamisho wa kwenda Dodoma ambapo aliweza kujiunga na shule ya msingi ya Mlimwa. Kisha baadaye shule ya Sekondari ya Mazengo na Chuo cha Ufundi cha Mazengo.
Katika ngazi ya familia, yeye ni mtoto wa mwisho (kwa baba akiwa mtoto wa 10) - na (kwa mama akiwa mtoto wa 6). Albert alifariki dunia mnamo tar. 28 Mei katika mwaka wa 2013 kwa hicho kinachoaminiwa kwamba alizidisha kipimo cha dawa za kulevya huko nchini Afrika Kusini. Ngwair ameacha mtoto mmoja.[1]
Kazi
Muziki
Ngwair alikuwa akiishi jijini Dar es Salaam, Tanzania ambako alikokutana na mtayarishaji mahiri wa mziki P. Funk Majani na kuanza kufanya naye kazi. Hiyo ilikuwa ni mwaka 2003 ambapo alitoa kibao cha kwanza kiitwacho 'Ghetto Langu,' wimbo uliompatia umaarufu mkubwa sana.
Mangwair pia aliwahi kushinda tuzo ya Kilimanjaro Music Awards kama mwana Hip Hop Bora wa mwaka 2005. Mwaka wa 2007 akatokea kwa wimbo wa kimya kimya akiwa na wana chemba. Katika Kimya Kimya anapagawisha.kwa sasa Ngwair anatesa na nyimbo inayotamba kwa jina washamba.
Albert Mangwair alifariki tarehe 28/5/2013 akiwa huko Afrika ya Kusini. Taarifa zinasema alifariki baada ya kutumia madawa ya kulevya lakini kuna utata kuhusu kilichosababisha kifo cha marehemu. [2]
Diskografia ya kuchaguliwa
Albamu
Nyimbo
- CNN ft Fid Q
- Mapenzi gani ft Lady Jaydee
- Aminia feat Inspecta Haruni, Mwana FA
- Birthday N'GE ft Mwasiti, TID & Mez B
- Speed 120 ft Chid Beenz
- TZ Hustler ft J-Son
- She performs ft TID
- Mafia ft. Jay Moe
- Bado nimo
- Salamu
- Mademu wangu
- Mida mibovu ft Juma Nature, Ferooz, P. Funk Majani, Dark Master & Jay Moe
- Kimya Kimya
- Nipe deal
- Singida Dodoma ft Dully Sykes
- Napokea simu
- Weekend
- Sikiliza
- Wife
- Tupo juu ft Squeezer & Steve RNB
- Ghetto langu
- Clubbin'
- She got a Gwan
Marejeo
- ↑ "Habari za Mangwair katika Blogu ya Anna Peter". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2013-06-17. Iliwekwa mnamo 2013-06-03.
- ↑ "Ripoti feki ya Ngwair katika VibeNews". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2013-06-13. Iliwekwa mnamo 2013-06-03.
Viuongo vya Nje
Makala hii kuhusu mwanamuziki/wanamuziki fulani wa Tanzania bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Mangwair kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |