Australasia ni neno la kutaja sehemu ya kusini magharibi ya Pasifiki inapopakana na Asia ya Kusini na Bahari Hindi. Inatazamiwa kama kanda la Australia na Pasifiki[1]. Si kawaida sana kimataifa lakini hueleweka hasa Australia na nchi za jirani penyewe.

Eneo la Australasia jinsi linavyoelezwa mara nyingi

Hasa Australia, New Zealand, Guinea Mpya na visiwa jirani vya Melanesia huhesabiwa humo. Wakati mwingine sehemu ya visiwa vya Indonesia vyahesabiwa humo pia.

Katika matumizi ya neno "Australasia" maeneo yake hungiliana na yale yanayotajwa kwa "Melanesia" na "Asia ya Kusini".

Neno lilitungwa na mtaalamu Mfaransa wa jiografia Charles de Brosses mwaka 1756 alipotaka kutofautisha eneo hili na Polynesia na Pasifiki ya Kusini-mashariki.

Kiutamaduni kuna tofauti kubwa ndani ya kanda hila lakini kijiografia kuna mambo ya pamoja kama vile wanyama aina za marsupialia au mimea ya ukoo wa mikalatusi.

Timu za Australia na New Zealand ziliwahi kugombea pamoaja kwa jina la "Australasia" kwenye michezo ya Olimpiki na Davis Cup.

Marejeo

hariri
  1. Kamusi ya KKS inatumia jina hili kwa umbo "Australesia" kwa maeneo yote ya Australia na Pasifiki; hii inaonekana ni kosa kwa sababu Australasia ni sehemu tu ya eneo linaloitwa "Oceania" kwa Kiingereza.