Awa Ehoura Tabitha ni mtangazaji wa nchini Ivory Coast na alikuwa mshauri maalum aliyesimamia mawasiliano kwa Rais Laurent Gbagbo. Ehoura alijulikana kwa kuwasilisha habari za saa saba mchana (7) na saa mbili usiku(2) kwenye media inayomilikiwa na serikali ya Première.[1][2]

Awa Ehoura Tabitha
Amekufa 5 Julai 2023
Abidjan Ivory Coast
Kazi yake Mtangazaji
Watoto 1

Alifutwa kazi kutoka kwa wadhifa wake na serikali ya Rais Alassane Ouattara | Allassane Ouattara mnamo Juni 2011 miezi miwili tu baada ya Gbagbo kuondoka madarakani.[3][4]

Kazi hariri

Ehoura alianza kazi yake ya utangazaji kwenye TV2 mwanzoni mwa miaka ya 1990. Chini ya ushauri wa Serge Pacôme Aoulou (SPA). Alipanda madaraja ya uongozi. Hadi kuwa mkurugenzi wa La Première na aliteuliwa mshauri maalum wa mawasiliano kwa Rais Laurent Gbagbo.[1]Alikuwa mtayarishaji wa programu "Raison d'Etat" wakati wa mgogoro wa Ivorian 2010-2011. Alifutwa kazi kutoka kwa nafasi yake na vyombo vya habari vya serikali miezi miwili tu baada ya Gbagbo kuondolewa madarakani na akaunti yake ya benki ilizuiliwa kwa muda pamoja na wafuasi wote wanaojulikana wa serikali ya Rais Gbagbo. Ehoura alipata mikataba na runinga za TV2, akiwasilisha programu ya gazeti na michezo.[5]

Marejeo hariri

  1. 1.0 1.1 "Abidjan: Awa Ehoura, ex DG de la Rti2 agonisante(Dédé) | AbidjanTV.net" (kwa en-US). 2017-08-06. Iliwekwa mnamo 2021-03-03. 
  2. "Côte d’Ivoire : Awa Ehoura n’est pas morte !". Ivoirebusiness.net (kwa Kifaransa). 2019-06-21. Iliwekwa mnamo 2021-03-03. 
  3. Serikpa, Carole (2014-05-02). "Côte d'Ivoire : Le régime Ouattara humilie les journalistes". L'œil de la Maison des Journalistes #MDJ (kwa fr-FR). Iliwekwa mnamo 2021-03-03. 
  4. "La grande interview : Awa Ehoura (Journaliste, ex-présentatrice du JT à la RTI) : "Je demande pardon à ceux que j’ai blessés"". Abidjan.net. Iliwekwa mnamo 2021-03-03. 
  5. CREDOCHRISTI (2019-06-20). "Côte d’Ivoire, Awa Ehoura : « Ça peut aller mieux par la grâce de Dieu ! | CREDOCHRISTI.COM" (kwa fr-FR). Iliwekwa mnamo 2021-03-03. 
  Makala hii kuhusu mtu huyo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Awa Ehuora kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.