Bamba la Karibi
Bamba la Karibi ni bamba la gandunia lililopo chini ya Amerika ya Kati na Bahari ya Karibi. Limepakana na mabamba ya Amerika ya Kaskazini, Amerika ya Kusini na Nazi (Cocos Plate). Eneo lake ni takriban milioni 3.2 km².
Mipaka yake na mabamba mengine ni mahali pa matetemeko ya ardhi na milipuko ya volkeno. Baharini mpaka huu unaonekana kwa pinde la visiwa vya Karibi.
Nadharia ya asili yake
haririNadharia ya asili yake inasema ya kuwa bamba hili lilikuwa sehemu ya juu ya bamba la Pasifiki. Wakati bamba la Atlantiki ilisukuma mabamba ya Amerika ya Kaskazini na Kusini kuelekea magharibi bamba hili la Karibi ilijisukuma juu ya bamba la Atlantiki. Kutokea kwa mlango wa nchi ya Amerika ya Kati kulitenganisha bamba hili na Pasifiki.
Viungo vya nje
hariri- NOAA Ocean Explorer
- Caribbean Plate formation PDF file Ilihifadhiwa 21 Oktoba 2006 kwenye Wayback Machine.