Kwa maana nyingine ya jina hili angalia hapa

Bamvua pamoja na upepo mkali katika mdomo wa mto inaweza kusababisha mafuriko kama hapa Hamburg, Ujerumani tarehe 13 Januari 2013
Wakati wa Mwezi mwandamu na Mwezi mpevu jua, mwezi na dunia ziko kwenye mstari mmoja na hapo nguvu za graviti zinaungana na kusababisha bamvua duniani.

Bamvua (ing. spring tide) inahusu kujaa na kupwa kwa maji ya bahari, hasa kujaa kukubwa. Mara nyingi neno hili hutumika na watu wa pwani na wavuvi. Kwa kawaida bamvua hutokea mara mbili kwa mwezi.

Bamvua inasababishwa na graviti ya jua na mwezi wakati dunia yetu, mwezi na jua ziko kwenye mstari nyoofu. Hii inaonekana kutokana na hali ya mwezi kuwa ama mwezi mwandamu au mwezi mpevu na karibu na siku hizi bamvua inatokea.

Kutegemeana na tabia za pwani mara nyingi bamvua haionekani sana yaani maji hujaa sentimita chache juu ya uwiano wa kawaida. Lakini kwenye mlango wa bahari kwa mfano kati ya kisiwa na bara, katika hori nyembamba au katika mdomo wa mto tofauti inaweza kuongezeka hasa ikiungana na upepo mkali wa kuelekea bara.

Makala hii kuhusu eneo fulani bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu eneo hilo kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Je, unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.


Usitaje majina ya madiwani na viongozi au maafisa wengine wa sasa maana wanabadilika haraka mno.