Bea Alonzo
Bea Alonzo (jina halisi: Phylbert Angellie Ranollo Fagestrom) ni mwigizaji wa filamu kutoka nchini Ufilipino. Alizaliwa mnamo tar. 17 Oktoba 1987. Baba yake ni Mwingereza, wakati mama yake ni Mfilipino. Yeye ni mmoja kati ya washirika wa ABS-CBN wenye vipaji na wanochipukia na wanaojulikana kama Star Magic katika mfululizo mzima wa vipindi vya televisheni vya Kifilipono.
Bea Alonzo | |
---|---|
| |
Jina la kuzaliwa | Phylbert Angellie Ranollo Fagestrom |
Alizaliwa | 17 Oktoba 1987 |
Jina lingine | Bea Alonzo |
Kazi yake | Mwigizaji |
Tovuti Rasmi | ya Bea Alonzo |
Maisha Yake
haririAkichipukia
haririBea Alonzo kama wasanii wengine, ndoto yaje ilikuwa ni kuwa msanii maarufu na mwenye mafanikio lukuki. Aliishi bila ya baba tangu ana miaka minne tu. Alijiunga katika mashindano ya urembo katika umri mdogo mno na alifanikiwa kwa kiasi katika jaribio hili. Katika mashindano ya urembo katika mji mdogo, mratibu wa masuala ya mitindo Oscar Peralta ndiye aligundua kipaji cha Bea. Baadae alimtambulisha kwa kiongozi wa ABS-CBN sekta ya vipaji Johnny Manahan aliyemtambulisha Bea kwenye Star Circle Batch 10. Hapo alipata mafunzo, ujuzi na uwezo mkubwa wa kuigiza ambao ulimsaidia baadae katika maigizo / vichekesho vya "K2BU".
Mafanikio
haririMnamo mwaka 2004, akiwa na miaka 15, Bea alicheza nafasi ya mwanasheria wa miaka 20 kama Katrina Argos katika tamthilia ya "Kay Tagaal Kang Hinintay". Nafasi iliyompatia tuzo yake ya kwanza ya muigizaji bora wa kike mwaka 2003 katika tuzo za PMPC Star Awards. Yeye alikuwa msanii mdogo kuzidi heshima aliyopata katika tuzo hiyo.
Kay Tagaal Kang Hinintay iliwaandalia John Lloyd na Bea timu ya wapenzi. Baada ya kufanikiwa katika tamthilia za "It Might Be You", "Ikaw Ang Lahat Sa Akin" na hii ya sasa "Maging Sino Ka Man" na filamu zao bora zaidi kama "My First Romance" (ambapo Bea alitangazwa kuwa "Muigizaji wa Bora wa Kike Mpya katika mudani ya Filamu" mwaka 2004 PMPC Star Awards [1]), "Now That I have You", "Close To You (film)" na hii ya "All About Love", walijulikana kama Timu Bora zaidi ya Mapenzi katika Nchi nzima.Baada ya"All About Love", kazi nyingine bora ya Filamu aliyofanya Bea ni "Pacifica Falapay".
Filamu Alizoigiza
haririOne More Chance (2007) kama Basya
All About Love (2006) kama Lia
Pacquiao, The Movie (2006) kama Jinkee Pacquiao
Close to You (2006) kama Marian
Dreamboy (2005) kama Cyd
Now That I Have You (2004) kama Betsy Rallos
My First Romance (2004) kama Bianca
Tamthilia Alizoigiza na Alizoshirikishwa
haririASAP (2007) kama Mshiriki Aliyekaribishwa
Maging Sino Ka Man Book 2 (2008) kama Jacqueline Madrigal Roxas
Maalaala Mo Kaya ("Barko" 2007) kama Camille
Wowowee (2007) kama Bea Alonzo (kashirikishwa)
Maging Sino Ka Man (2006-2007) kama Jackie Madrigal
Ikaw Ang Lahat Sa Akin (2005) kama Jasmin Cruz Fontanilla
It Might Be You (2003-2004) kama Cielo San Carlos
Kay Tagaal Kang Hinintay (2002-2003) kama Katrina Argos
K2BU (2002) kama Dianne
John N Shirley (2006) kama Bea
Komiks ("Pedro Penduko" 2006) kama Carmela
Your Song ("Ok Lang" 2006) kama Sandy
Star Magic Presents ("Miss ... Mistress" 2006) kama Monica
Maalaala Mo Kaya ("Palaisdaan" 2006) kama Meya Lina Bagasina
Komiks ("Bampy" 2006) kama Mkuu Wa Shule
Maalaala Mo Kaya ("Roses" 2006) kama Heny
Your Song ("You Win The Game" 2006) kama Marnie
Komiks ("Sa Mga Kamay Ni Hilda" 2006) kama Hilda
Bora (2006) kama Tuesday
Bora (2005) kama Tuesday
Bida si Mister, Bida si Misis (2004)
OK Fine Whatever (2004) kama Dr. Donna
Bida si Mister, Bida si Misis (2003) kama Katrina Legarda
Whattamen ("Disco Kids" 2003") kama Caramel
Maalaala Mo Kaya ("Lapis" 2003) kama Carol
Arriba! Arriba! (2003) kama Belinda
Wansapanataym ("Magic Salamin" 2003) kama Winnie
Star Studio ("Suyuan sa Lalawigan" 2003) kama Lucia
Star Studio ("Magnanakaw" 2002) kama Msichana Tajiri
Tuzo
hariri2007 USTV Students Choice Awards, Muigizaji bora wa kike katika Maging Sino Ka Man
2006 Yes Magazine Awards, Timu ya Wapenzi Maarufu Zaidi pamoja na John Lloyd Cruz
2006 Yes Magazine Awards, Nyota Mdogo wa Kike
2006 ANAK TV Seal Award, Miongoni Mwa Wasichana 10 Binafsi Wenye Mvuto zaidi
2005 Miss FAMAS Screen Idol, FAMAS
2004 Princess of RP Movies for “Now That I Have You", Guillermo Mendoza
2004 Mugizaji mpya Bora wa kike katika filamu ya “My First Romance", Star Awards for Movies
2003 Timu ya Wapenzi Maarufu katia filamu za RP pamoja na John Lloyd Cruz na Guillermo Mendoza
Marejeo
hariri- ↑ "Nakala iliyohifadhiwa". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2007-09-30. Iliwekwa mnamo 2007-11-08.
Viungo Vya Nje
hariri- Tovuti Rasmi ya Bea Alonzo
- Bea Alonzo at the Internet Movie Database
- Bea Alonzo Ilihifadhiwa 13 Desemba 2007 kwenye Wayback Machine. Katika Pinoy Central