Rebbeca Marie Gomez (anajulikana kama Becky G; alizaliwa Machi 2, 1997) ni mwanamuziki, mtunzi wa nyimbo na muigizaji kutoka nchini Marekani.

Hii ni picha ya Becky G

Kwa mara ya kwanza Gomez aliweza kutambulika kutokana na hali yake ya kurusha nyimbo mbalimbali maarufu katika mitandao huku akiwa amezirudia kuimba na hii ilikuwa mnamo mwaka 2011. Moja ya video yake iliweza kumvutia mtayarishaji wa nyimbo kwa jina la Dr. Luke, ambaye alimsaidia kujiunga na lebo za kurekodia za Kemosabe Records na RCA Records. Huku akiwa anajitegemea Gomezi aliweza kushirikiana na wasanii kama will.i.am, Cody Simpson na Cher Lloyd.

Wimbo wake wa kwanza kutoa "Becky from the Block" (2013) uliwea kupata umaaufu mkubwa na kupokewa vizuri na wadau wa muziki pia alitoa wimbo wa Play It Again ndani ya mwaka huohuo. Aliendelea kuto nyimbo mbalimbali hadi akawa maarufu nchini Marekani.

Makala hii kuhusu mwanamuziki/wanamuziki fulani wa Marekani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Becky G kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.