Bendera ya Angola
Bendera ya Angola ina milia miwili ya kulala. mlia wa juu ni nyekundu na mlia wa chini ni nyeusi. Katikati kuna nembo ya njano.
Jinsi ilivyo katika nchi mbalimbali za Afrika bendera ya chama tawala imebadilishwa kidogo na kutangazwa kuwa bendera ya taifa. Katika Angola ni chama cha MPLA kilichoshinda baada ya vita ya wenywewe kwa wenyewe na kubadilisha bendera yake hivyo.
Rangi ya nyekundu ilimaanisha usoshalisti, nyesusi bara na watu wa Afrika.
Baadaye maelezo kwa ajili ya nyekundu yalibadilishwa kumaanisha jitihada na damu yaliyomwagika kwa ajili ya uhuru wa taifa.
Alama ndani ya bendera inafanana na mundu na nyundo nembo ya Umoja wa Kisovyet. Hapa ni nusu ya gurudumu meno, panga na nyota. Bendera ilianzishwa rasmi tarehe 11 Novemba 1975 offiziell eingeführt.
Alternativvorschlag
haririTangu 2003 kuna pendekezo la bendera jipya isiyokumbusha itikadi wala damu na vita.