Open main menu

Umoja wa Kisovyeti

(Elekezwa kutoka Umoja wa Kisovyet)
Bendera ya Umoja wa Kisovyeti
Picha:Kolkhoznitsa.jpg
Sanamu ya mfanyakazi wa kiwandani pamoja na mkulima wa kike mjini Moscow

Umoja wa Kisovyeti (kwa Kirusi: Советский Союз, tamka: sovjetskii soyuz, kifupi cha: Umoja wa Jamhuri za Kisovyeti za Kijamii) ilikuwa nchi kubwa duniani kati ya 1922 hadi 1991. Mara nyingi illitwa pia "Urusi" lakini ilijumlisha Urusi pamoja na maeneo mengine yaliyotwaliwa na Urusi katika mwendo wa historia kabla ya kutokea kwa Umoja wa Kisovyeti yaliyoendelea kuwa nchi huru baadaye.

Ilianzishwa katika Mapinduzi ya Urusi ya 1917 ikachukua nafasi ya Milki ya Urusi ya awali. Umoja wa Kisovyeti ulitawaliwa na chama cha kikomunisti. Wakomunisti waliamua kutawala Dola la Urusi la awali kwa muundo wa shirikisho wakaunda jamhuri mbalimbali kufuatana na mataifa ndani ya eneo hili kubwa.

Kikatiba jamhuri hizi zote zilikuwa nchi huria lakini hali halisi zilitawaliwa zote kutoka makao makuu ya chama cha kikomunisti huko Moscow. Katiba ilipata umuhimu tangu 1989 wakati wa mwisho wa utawala wa Wakomunisti ambako jamhuri zote zilitafuta uhuru wao zikaachana na Umoja.

Mwaka 1991 jamhuri wanachama za mwisho Urusi, Belarus na Ukraine ziliamua kumaliza Umoja wa Kisovyeti.

ViongoziEdit

Makatibu Wakuu wa Chama cha KikomunistiEdit

Jamhuri za Umoja wa KisovyetiEdit