Bendera ya Denmark
Bendera ya Denmark au "Danebrog" ni ya rangi nyekundu yenye msalaba mweupe ndani yake. Muundo wa bendera hii imechukuliwa kama mfano na nchi zote za Skandinavia.
Danebrog inasemekana kuwa bendera ya kitaifa ya kale ya dunia inayoendelea kutumiwa tangu karne ya 14 BK hado leo bila mabadiliko.
Hadithi ya kale inasema ya kwamba wakati wa vita ya Denmark huko Estonia bendera hii ilianguka kutoka angani mwaka 1219 wakati wa kipindi kigumu katika mapigano hivyo ikawapa Wadenmark moyo na kuleta ushindi.