Estonia (kwa Kiestonia: Eesti au Eesti Vabariik) ni nchi ya Kibalti katika Ulaya ya Kaskazini. Imepakana na Latvia na Urusi.

Estonia


Ramani ya Estonia

Finland iko ng'ambo ya Kidaka cha Ufini cha Bahari ya Baltiki na watu wake wana asili moja na Waestonia.

Mji mkuu ni Tallinn unaojulikana pia kwa jina la Reval.

Historia hariri

Kwa muda mrefu Estonia ilikuwa chini ya Wajerumani, Wadani na Waswidi, halafu sehemu ya Dola la Urusi.

Katika miaka 1918-1940 ilikuwa jamhuri halafu miaka 1940-1991 mwanachama wa Umoja wa Kisovyeti.

Baada ya umoja huo wa majimbo 15 kusambaratika, Estonia ilijitangaza nchi huru.

Estonia imekuwa nchi mwanachama ya Umoja wa Ulaya tangu tarehe 1 Mei 2004.

Watu hariri

Lugha rasmi ni Kiestonia ambacho ni lugha mama ya 69.1% ya wakazi na karibu sana na Kifini. Karibu robo husema Kirusi.

Upande wa dini, kadiri ya sensa ya mwaka 2011, 54.14% hawana yoyote. Wakristo Waorthodoksi ni 16.5%, Walutheri ni 9.91%, mbali ya madhehebu mengine yasiyofikia pekepeke 1%.

Tazama pia hariri

Viungo vya nje hariri


Nchi za Umoja wa Ulaya  
Austria | Bulgaria | Eire | Estonia | Hispania | Hungaria | Italia | Kroatia | Kupro | Latvia | Lituanya | Luxemburg | Malta | Polandi | Slovakia | Slovenia | Romania | Ubelgiji | Ucheki | Udeni | Ufaransa | Ufini | Ugiriki | Uholanzi | Ujerumani | Ureno | Uswidi
  Makala hii kuhusu maeneo ya Ulaya bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Estonia kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.