Bendera ya Moroko
Bendera ya Moroko ni nyekundu ina nyota ya kijani yenye pembe tano katikati. Ilitumiwa rasmi tangu 17 Novemba 1915 lakini ina historia ya karne kadhaa nchini.
Rangi nyekundu ilionyeshwa tangu karne ya 17 na watawala wa familia ya Waalawi kwa sababu wanadai ni sehemu ya ukoo wa mtume Muhamad na nyekundu ni alama ya ukoo huo.
Wakati wa Moroko kuwa nchi lindwa chini ya Ufaransa nyota ya pembetano iliingizwa.