Bendera ya Nigeria
Bendera ya Nigeria ina milia ya kusimama mitatu, miwili ya nje ni kijani na ile ya katikati ni nyeupe.
Bendera ilipatikana katika mashindano ya kitaifa kabla ya uhuru mwaka 1959 na kuonekana rasmi mara ya kwanza tarehe 1.10.1960. Mshindi aliyetunga bendera hii alikuwa mwanafunzi wa uhandisi Michael Taiwo Akinkunmi kutoka Ibadan.
Rangi ya kijani inatakiwa kuonyesha misitu na mashamba yenye rutuba na mlia mweupe humaanisha amani.