Benn Haidari ni mpishi na mwanasiasa, aliazaliwa tarehe 6 Machi 1949 katika kijiji cha Mbeni huko Ngazija visiwa vya Komoro. Mjomba wake Maalim Said Ilyas akamchukua Zanzibar mwaka wa 1953. Akamaliza masomo yake Fidel Castro Secondary School na kuhamia Ufini 1968.

Bw. Haidari alisomea mambo ya upishi kwenye visiwa vya Aland huko Ufini na akawa katika mpishi mkubwa na wa mwanzo wa kufanya filamu za mapishi katika Televisheni za Skandinavia mnamo mwaka 1988.

Filamu yake ya kwanza ni Pengine nitakuwa mpishi wa pizza na baadaye akafanya filamu 12 za mapishi ya dunia pamoja na mapishi ya kizanzibari, k.m. Samaki wa kupaka na Mkate wa kusukuma.

Mwaka 2005 Bw. Haidari alialikwa Ujapani Tokyo kuonesha mapishi yake katika television ya ujapani.

Kitabu chake cha kwanza cha mapishi kilitolewa tarehe 25 Januari 2006.

Bw. Haidari aligombania Ubunge katika visiwa vya Åland mwaka wa 2007.

Marejeo

hariri

Modern-Zanzibar-Cuisine-Benn-Haidari