Komori

nchi huru iliyo kwenye visiwa katika Bahari ya Hindi karibu na pwani ya mashariki ya Afrika
(Elekezwa kutoka Komoro)
Umoja wa Komori (Kiswahili)
Udzima/Uzima wa Komori (Kikomori)
Bendera ya Komori Nembo ya Komori
(Bendera ya Komori) (Nembo ya Komori)
Lugha rasmi Kifaransa
Mji Mkuu Moroni
Mji Mkubwa Moroni
Serikali Shirikisho la Jamhuri
Rais Azali Assoumani
Waziri Mkuu
Eneo km² 1,659
Idadi ya wakazi 850,688 (2018)
Wakazi kwa km² 457
Uchumi nominal Bilioni $1.179
Uchumi kwa kipimo cha umma $1,349
Pesa Frank ya Komori
Kaulimbiu "Umoja - Mshikamano - Maendeleo"
Wimbo wa Taifa Udzima wa ya Masiwa(Uzima wa Visiwa)
Komori katika Afrika
Saa za Eneo UTC +3 (Wakati wa Afrika Mashariki)
Mtandao .km
Kodi ya Simu +269


Komori (kwa Kiswahili pia: Visiwa vya Ngazija; kwa Kikomori: قمر, Komori, kwa Kifaransa: Comores) ni nchi huru kwenye funguvisiwa katika Bahari Hindi upande wa Mashariki wa Afrika. Iko katika Kanali ya Msumbiji kaskazini kwa Madagaska na mashariki kwa Msumbiji.

Union des Comores
Udzima wa Komori

اتحاد القمر

Umoja wa Komori
Bendera ya Komori Nembo ya Komori
Bendera Nembo
Kaulimbiu ya taifa: Unité - Justice - Progrès
(Umoja – Haki - Maendeleo)
Wimbo wa taifa: Udzima wa ya Masiwa
Lokeshen ya Komori
Mji mkuu Moroni
11°41′ S 43°16′ E
Mji mkubwa nchini Moroni
Lugha rasmi Shikomor, Kiarabu, Kifaransa
Serikali Shirikisho la Jamhuri
Ikililou Dhoinine
Uhuru
- tarehe
kutoka Ufaransa
6 Julai 1975
Eneo
 - Jumla
 - Maji (%)
 
2,170 km² (ya 167)
--
Idadi ya watu
 - 2002 kadirio
 - Msongamano wa watu
 
596,202 (ya 158)
275/km² (275)
Fedha Frank ya Komori (KMF)
Saa za eneo
 - Kiangazi (DST)
EAT (UTC+3)
not observed (UTC+3)
Intaneti TLD .km
Kodi ya simu +269

-


Jina limetokana na lugha ya Kiarabu ambapo Juzur al-Qamar (جزر القمر) linamaanisha "visiwa vya mwezi".

Katika Afrika iko kati ya nchi tatu ndogo kabisa.

  • Pesa: 1 Frank ya Komori (FC) = 100 centimes. 1€ = 491,9677 FC
  • Sikukuu ya Taifa: 4 Julai

Jiografia hariri

 
Ramani ya Komori

Komori ina visiwa vitatu vikubwa: Grande Comore (Ngazidja), Anjouan (Nzwani) na Moheli (Mwali). Kisiwa cha Mayotte ni sehemu ya funguvisiwa kijiografia lakini kisiasa ni sehemu ya Ufaransa kwa sababu wakati wa kupata uhuru watu wa Mayotte walitamka kwa kura nyingi (73%) ya kwamba wanataka kukaa na Ufaransa. Lakini Komori inadai ni sehemu ya eneo lake.

Komori ni sehemu ya bara la Afrika. Ina pia visiwa mbalimbali vidogo.

Hali ya hewa ni ya kitropiki. Kuna mvua miezi yote.

Kitovu cha kisiwa kikubwa zaidi (Grande Comore) ni mlima wa volkano hai Karthala wenye mita 2,461 juu ya UB. Safari iliyopita Karthala ililipuka mwaka 1977 ikaharibu kijiji kimoja.

Miji hariri

Miji mikubwa ni (wakazi mwaka 2005): Moroni 42.872, Mutsamudu 23.594, Fomboni 14.966, Domoni 14.509 na Tsémbehou 11.552.

Historia hariri

Visiwa vya Komori vimekaliwa na watu mbalimbali kutoka Afrika na Asia Kusini katika historia ndefu. Wanaakiolojia walitambua mabaki ya makazi ya watu kutoka karne ya 6 kwenye kisiwa cha Nzwani lakini haijulikani kama watu walitangulia kufika mapema bila kuacha mabaki ya kutambulika.

Waswahili wa kwanza walifika kama sehemu ya uenezi wa Wabantu tangu karne ya 9 BK.

Kipindi cha kwanza huitwa kipindi cha Dembeni (karne ya 9 - 10) ambako Waswahili walianzisha kijiji kimoja katika kila kisiwa.

Wakati wa karne ya 11 hadi ya 15 biashara iliongezeka na Madagaska pia na wafanyabiashara kutoka Uarabuni. Vijiji vidogo vikaongezeka na vijiji vya awali vikakua vikawa miji.

Kumbukumbu ya wenyeji hutaja mara nyingi majina ya Waarabu kutoka Yemen na Saba' kama mababu wa koo asilia lakini hakuna uhakika kama kumbukumbu hizo zinalingana na historia halisi.

Athira ya Kiarabu na ya Kiislamu ikaongezeka kutokana na biashara ya watumwa, dhahabu na pembe za ndovu kati ya Afrika ya Mashariki na nchi za Kiislamu.

Waarabu na Waajemi walijenga vituo kwa ajili ya biashara yao pamoja na misikiti na kueneza dini ya Uislamu kwenye visiwa.

Hata kama Komori si karibu sana na pwani, hata hivyo kutokana na mwendo wa upepo ni kituo muhimu cha jahazi kwenye safari kati ya Kilwa na Msumbiji iliyokuwa bandari kuu ya dhahabu ya Zimbabwe.

Siasa hariri

Kufuatana na katiba ya uhuru ya mwaka 1975 Komori ilitangazwa kuwa jamhuri ya Kiislamu. Serikali zilipinduliwa mara kwa mara na wanajeshi au na mamluki.

Katiba mpya ya mwaka 2001 imeondoa tabia ya kidini ya dola na iliunda utaratibu wa urais kuzunguka kati ya visiwa vitatu vikubwa.

Katika muundo huo rais wa jamhuri atateuliwa kila baada ya miaka minne kutoka kisiwa tofauti.

Katika uchaguzi ya mwaka 2002 rais Azali Assoumani alichaguliwa kutoka kisiwa cha Ngazidja (Komori Kuu). Katika uchaguzi wa 2006 rais amechaguliwa kati ya wagombea kutoka kisiwa cha Anjouan. Wananchi wa Anjouan walipiga kura ya kwanza. Wagombea watatu wenye kura nyingi wameteuliwa na kusimamishwa mbele ya wapiga kura wa visiwa vyote watakaomchagua rais wa jamhuri.

Rais wa mwaka 2010 alitoka katika kisiwa cha Moheli, baadaye tena rais kutoka Ngazidja, n.k.

Katika uchaguzi wa 2010 ndiye Ikililou Dhoinine aliyepata kura nyingi.

Watu hariri

Watu wa Komori ni mchanganyiko wa Waarabu, Wamadagaska, Waafrika wa bara ambao mababu walikuwa watumwa, Wahindi na Wazungu kadhaa.

Kutokana na uhaba wa ajira Wakomori wengi wamehamia nje, hasa Madagaska.

Wakazi wengi ni Waislamu (98%, hasa Wasunni), wakifuatwa na Wakristo (2%). Karibu nusu ya wananchi wote hawajui kusoma.

Ina lugha rasmi tatu ambazo ni Kifaransa, Shikomor (inayofanana na Kiswahili) na Kiarabu.

Nje ya Kifaransa, Kiarabu na Kimalagasy Sanifu, kuna lugha tatu za asili ambazo huzungumzwa na Wakomori, yaani Kimwali, Kindzwani na Kingazidja ambazo ziko karibu na Kiswahili.


Uchumi hariri

Komori ni kati ya nchi maskini zaidi duniani. Kilimo, uvuvi, uwindaji na misitu ni misingi ya uchumi wote.

Barabara na mawasiliano ya meli au ndege ni haba, idadi ya watu inakua haraka, elimu ni duni; haya yote yanasababisha kudumu kwa uchumi wa kijungujiko na uhaba wa ajira. 80% ya wafanyakazi wote wanashughulika kilimo.

Tazama pia hariri

Viungo vya nje hariri


Nchi za Afrika  
Afrika ya Kati (Jamhuri ya) | Afrika Kusini | Algeria | Angola | Benin | Botswana | Burkina Faso | Burundi | Cabo Verde | Chad | Cote d'Ivoire | Eritrea | Eswatini | Ethiopia | Gabon | Gambia | Ghana | Guinea | Guinea Bisau | Guinea ya Ikweta | Jibuti | Kamerun | Kenya | Komori | Kongo (Jamhuri ya) | Kongo (Jamhuri ya Kidemokrasia ya) | Lesotho | Liberia | Libya | Madagaska | Malawi | Mali | Misri | Morisi (Visiwa vya) | Mauritania | Moroko | Msumbiji | Namibia | Niger | Nigeria | Rwanda | Sahara ya Magharibi | Sao Tome na Principe | Senegal | Shelisheli | Sierra Leone | Somalia | Sudan | Sudan Kusini | Tanzania | Togo | Tunisia | Uganda | Zambia | Zimbabwe
Maeneo ya Afrika ambayo ni sehemu za nchi nje ya Afrika
Hispania: Kanari · Ceuta · Melilla | Italia: Pantelleria · Pelagie | Ufaransa: Mayotte · Réunion | Uingereza: · St. Helena · Diego Garcia | Ureno: Madeira
  Makala hii kuhusu maeneo ya Afrika bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Komori kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.