"Betty Aloyce Kazimbaya" (amezaliwa tar. 4 Machi, 1973[1]) ni jina la mwigizaji wa filamu kutoka nchini Tanzania. Anajulikana zaidi kwa kucheza uhusika wa Mwanaidi kutoka katika mfululizo wa televisheni maarufu wa Siri ya Mtungi (2012)[2].

Taswira ya Mwanaidi (uhusika umechezwa na Betty Kazimbaya)

Pia amecheza kama Mama Aisha (Samaki Mchangani—2014[3]), Mama Mwandenga (Going Bongo—2015), Mama Tumaini (Binti—2021[4]).

Mwaka wa 2021, amepata kuonekana katika tamthilia ya "Haikufuma" akicheza uhusika wa "Jalia."

Vilevile amewahi kuwa Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Sanaa za Maonyesho Tanzania.[5]

Filamu alizocheza hariri

Caption text
Na. Jina la filamu Uhusika Maelezo
1 Neema 1998—filamu ya kwanza
2 Kijiweni 2000
3 Shangazi 2002
4 Wacha Masihara 2012—2014, mchezo wa redio wa Hypermedia
5 Siri ya Mtungi Mwanaidi 2012
6 Samaki Mchangani Mama Aisha 2014
7 Going Bongo Mama Mwandenga 2015
8 Binti Mama Tumaini 2021

Marejeo hariri

  1. "Betty Kazimbaya". IMDb. Iliwekwa mnamo 2021-08-26. 
  2. Siri ya Mtungi (TV Series 2012) - IMDb (kwa en-US), iliwekwa mnamo 2021-08-26 
  3. Samaki Mchangani (Short 2014) - IMDb (kwa en-US), iliwekwa mnamo 2021-08-26 
  4. Binti (2021) - IMDb (kwa en-US), iliwekwa mnamo 2021-08-26 
  5. Going Bongo (2015) - IMDb (kwa en-US), iliwekwa mnamo 2021-08-26