Bexagliflozin, inayouzwa kwa jina la chapa Brenzavvy kati ya mengine, ni dawa inayotumika kutibu kisukari cha aina ya 2.[1] Inatumika pamoja na lishe maalumu na mazoezi[1] na inachukuliwa kwa mdomo.[1]

Madhara yake ya kawaida ni pamoja na maambukizi ya ya kuvu ukeni, maambukizi ya njia ya mkojo na kuongezeka kwa mkojo.[1] Madhara yake makubwa yanaweza kujumuisha upungufu wa insulini unaosababisha asidi ya keto kwa wagonjwa wa kisukari (ketoacidosis ya kisukari), kukatwa kiungo, sukari ya chini ya damu, Fournier's gangrene (kifaafa cha Fournier, ambayo ni aina nadra lakini hatari ya gangrini (kifo cha tishu) inayosababishwa na maambukizi ya bakteria yanayoathiri sehemu za siri, eneo la kinena, na wakati mwingine makalio), na matatizo ya figo.[1] Haipendekezwi kuitumia wakati wa mwisho wa ujauzito.[1] Dawa hii ni kizuizi cha mchukuzi-mshiriki wa sodiamu na glukosi 2 (sodium-glucose cotransporter 2 (SGLT2)inhibitor).[1]

Bexagliflozin iliidhinishwa kwa ajili ya matumizi ya kimatibabu nchini Marekani mwaka wa 2023.[1] Gharama yake nchini Marekani haikuwa wazi kufikia mapema mwaka wa 2023.[2]

Marejeo

hariri
  1. 1.0 1.1 1.2 1.3 1.4 1.5 1.6 1.7 "Archive copy" (PDF). Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo (PDF) mnamo 2023-03-06. Iliwekwa mnamo 2023-03-07.{{cite web}}: CS1 maint: archived copy as title (link)
  2. "FDA Approves New Drug for Type 2 Diabetes". Formulary Watch (kwa Kiingereza). Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 7 Februari 2023. Iliwekwa mnamo 1 Mei 2023.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  Makala hii kuhusu mambo ya tiba bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Bexagliflozin kama sababu yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.