Bi Sloane
Bi Sloane ni filamu ya kusisimua ya kisiasa iliyochezwa mwaka 2016 iliyoongozwa na John Madden na iliyoandikwa na Jonathan Perera.
Nyota wa filamu hiyo ni Jessica Chastain, Mark Strong, Gugu Mbatha-Raw, Michael Stuhlbarg, Alison Pill, Jake Lacy, John Lithgow, na Sam Waterston.
Filamu hiyo inamfuata Elizabeth Sloane, mshawishi mkali, ambaye anapigana katika jaribio la kupitisha sheria ya udhibiti wa bunduki. lakini, anaachwa hoi wakati chama pinzani kinachimba sana maisha yake ya binafsi.