Bunduki ni silaha inayorusha risasi dhidi ya shabaha yake. Ndani ya bunduki inatokea mlipuko wa baruti na gesi joto za mlipuko zinasukuma risasi kufuata mwelekeo wa kasiba yake. Kutokana na sifa hii huitwa pia silaha ya moto. Kasiba ya bunduki za kisasa huwa na mifuo ndani yake inayosababisha risasi kuzunguka; inaendelea kuzunguka baada ya kutoka nje ya kasiba na mwendo huu unatunza mwelekeo wake. Kipenyo cha risasi ni sawa na kipenyo cha ndani cha kasiba hivyo risasi inagusa kasiba wakati wa kufyatuliwa.

Askari na bunduki
Aina mbalimbali za bunduki
TKB-059.

Bunduki ya kisasa huwa na akiba ya ramia katika chemba yake isipokuwa silaha kadhaa za kuwinda. Silaha za kijeshi huwa na chemba zonazoshika risasi zaidi ya 100.

Aina za bunduki

hariri

Kwa kawaida neno "bunduki" linataja silaha za moto zenye kasiba ndefu zinazoshikwa mikononi.

  • Gobori ni mtangulizi wa bunduki ambalo risasi na baruti zinaingizwa kupitia mdomo wake katika kasiba. Kasiba yake ni nyororo, haina mifuo. Kwa hiyo haiwezi kulenga kwa umakini. Inapiga mara moja tu halafu ni lazima kuijaza upya. Aina hii ni silaha ya kihistoria lakini hupatikana pia kama silaha inayotengenezwa nyumbani.
  • Bunduki kubwa zaidi zinazosimama kwa magurudumu huitwa mzinga.
  • Bunduki ndogo yenye kasiba fupi ni bastola.
  • Bunduki kubwa kiasi inayofyatua risasi nyingi wakati moja ni bombomu (au: mzinga wa bombom; bunduki ya mtombo; bunduki ya rashasha).
  • Aina hii kama ndogo zaidi ni bunduki ya nusu mtombo.
  • Bunduki ya upepo inayotumia nguvu ya gesi yenye shinikizo bila mlipuko. Silaha ndogo ya aina hii inapata shinikizo kwa kukandamiza hewa katika chemba cha bunduki. Aina zenye nguvu zinatumia ramia isiyo na baruti bali na gesi iliyokandamizwa ndani yake. Faida yake ni hazina kelele kubwa.
  • Bunduki ya marisau hutumiwa kwa kuwinda wanyama ikifyatua risasi nyingi ndogondogo. Ni rahisi zaidi kushika shabaha lakini haipigi mbali.

Viungo vya nje

hariri
 
Wikimedia Commons ina media kuhusu:
  Makala hii kuhusu mambo ya teknolojia bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu mada hiyo kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.