Billboard 200 ni safu ya kutaja albamu za muziki na ma-EP 200 zenye-mauzoya juu huko nchini Marekani. Safu hii huchapishwa kila wiki na jarida la Billboard. Mara kwa mara hutumiwa kufikisha au kutoa habari za umaarufu wa msanii au kundi la wasanii. Mara kwa mara, rekodi bora itakumbukwa kwa kufika kwake katika "nafasi ya kwanza", hizo albamu zao ambazo zimeuza zaidi kuliko nyingine angalau katika wiki moja.

Chati hii imeegemea sana upande mmoja tu wa mauzo (mauzo ya rejareja na yale ya dijitali) ya albamu huko nchini Marekani. Mauzo ya nyimbo yanaanza siku ya Jumatatu na kuishia Jumapili. Chati mpya inachapishwa kwa Alhamis inayofuata ikiwa na tarehe ya toleo lijalo la Jumamosi.

Mfano:
Jumatatu 1 Januari — wiki ya mauzo ya nyimbo yanaanza
Jumapili 7 Januari — wiki ya mauzo ya nyimbo yanaisha
Alhamisi 11 Januari — chati mpya zinachapishwa, ikiwa pamoja na tarehe ya toleo la Jumamosi tar. 20 Januari.

Viungo vya Nje hariri