Billboard Hot 100 ni jina linalotumika kutaja viwango vya muziki, yaani, chati za single maarufu, na kadhalika ambazo hutolewa kila wiki na gazeti la Billboard la nchini Marekani. Chati hutegemea kwa wimbo kupigwa sana maredioni au kufanya vizuri mauzoni; wiki ya mauzo ya wimbo huanza Jumatatu na kuisha Jumapili; wakati kupigwa redioni kwa nyimbo-inaanza kuanzia Jumatano hadi Jumanne. Chati mpya zinakusanywa na zinatolewa rasmi katika umma na Billboard mnamo Alhamisi. Kila chati imewekewa tarehe ya "wiki inayoishia" baada ya Jumamosi.

Nembo ya Billboard Hot 100
Mfano:
Jumatatu, 1 Januari – mauzo ya wiki ya nyimbo-yanaanza
Jumatano, 3 Januari — wiki ya kupigwa sana-inaaza
Jumapili, 7 Januari – mauzo ya wiki ya nyimbo-yanaisha
Jumanne, 9 Januari – wiki ya kupigwa sana-inaisha
Alhamisi, 11 Januari – chati mpya zinatolewa, na tarehe ya kutolewa Jumamosi, 20 Januari.

Vyanzo

hariri

Marejeo

hariri

Viungo vya Nje

hariri