Bodi ya Wahandisi wa Tanzania

Bodi ya Wahandisi wa Tanzania ni chombo kilichoanzishwa chini ya Sheria ya Usajili wa Wahandisi, Namba 15 ya mwaka 1997. Bodi imepewa jukumu la kuangalia na kudhibiti shughuli za uhandisi na mwenendo wa wahandisi na mashirika ya kandarasi za uhandisi nchini Tanzania, kupitia usajili wa wahandisi na mashirika ya kandarasi ya uhandisi.[1]

Bodi hii inahusika na utaratibu wa kuratibu maadili ambapo inalenga kudhibiti shughuli za uhandisi na mwenendo wa wahandisi na mashirika ya ukandarasi. Hivyo Bodi imeunda kanuni ambazo ndio msingi wa mfumo wa utendaji wa kazi zote za kihandisi kwani inaelezea viwango vya mwenendo wa kuzingatiwa na wahandisi na Mashirika ya kandarasi. Kanuni hizi ndio zinazounda mfumo mahususi kwa ajili ya kusimamia Ukweli, Uaminifu, uadilifu na kuheshimu uhai na maisha ya binadamu na ustawi wa jamii, usawa, uwazi, uwezo wa utendaji na uwajibikaji, ubora wa uhandisi na ulinzi na utunzaji wa Mazingira na maendeleo endelevu.[2]

Marejeo

hariri
  1. "Nakala iliyohifadhiwa". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2020-02-21. Iliwekwa mnamo 2020-02-21.
  2. https://constructionreviewonline.com/2017/04/registering-as-a-professional-engineer-with-engineers-registration-board-of-tanzania/