Bogaletch "Boge" Gebre (1960 – 2 Novemba 2019)[1] alikuwa mwanasayansi na mwanaharakati kutoka Ethiopia.

Bogaletch Gebre

Mnamo mwaka 2010, gazeti la The Independent lilimuelezea kama mwanamke aliyeanzisha mapambano ya wanawake wa Ethiopia."[2] Akiwa na dada yake Fikirte Gebre, Gebre alianzisha KMG Ethiopia, ambayo awali iliitwa Kembatti Mentti Gezzima-Tope (Kembatta Women Standing Together).[3] Hisani hii husaidia wanawake katika maeneo mbalimbali, ikiwemo kupinga na kuepusha ukeketaji wa wawanawake (FGM) na utekaji wa bibi harusi, unaohusisha ubakaji wa wanawake wadogo ili kuwalazimisha waingie katika ndoa.[4] Kwa mujibu wa kamati ya kitaifa ya mila na jadi za Ethiopia, matendo hayo yalikuwa ndio msingi wa asilimia 69 ya ndoa zote nchini humo kwa mwaka 2003.[2]

Gazeti la The Independent linaripoti kuwa shirika hilo limepunguza utekaji wa bi harusi huko Kembatta kwa asilimia 90, pia gazeti la The Economist linasema kuwa shirika hilo limechangia kupunguza ukeketaji wa wanawake kutoka asilimia 100 mpaka asilimia 3.[2][5] Mnamo mwaka 2005, Gebre alitunukiwa tuzo ya North-South Prize ya 2005 na mwaka 2007 alipewa tuzo ya Jonathan Mann kwa ajili ya afya ya ulimwengu na haki za binadamu.[6] Kutokana na mchango wake kwa maendeleo ya Afrika, Boge alipewa tuzo ya King Baudouin International Development Prize mwezi mei, mwaka 2013.[3][5][7]

Historia

hariri

Yeye mwenyewe alikuwa mhanga wa ukeketaji akiwa na umri wa miaka 12, Gebre alinyimwa haki ya kupata elimu rasmi (kiin. Formal education) na baba yake, lakini alikuwa akioroka nyumbani ili kwenda shule ya wamishonari.[3][8] Mwishowe, alisomea mikrobiolojia huko Yerusalemu kabla ya kujiunga na chuo kikuu cha Massachusetts Amherst kwa udhamini wa Fulbright scholarship.[2] Akiwa nchini Marekani, alianzisha shirika lake la kwanza la hisani, Development through Education, kupitia hilo shirika wanafunzi wa shule za sekondari na vyuo vikuu vya Ethiopia walipokea kiasi cha dola za kimarekani 26,000 kwa ajili ya vitabu vya kiufundi.[9]

Marejeo

hariri
  1. "Ethiopian Women Rights Advocate Passes Away". www.ezega.com. Iliwekwa mnamo Nov 12, 2019.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  2. 2.0 2.1 2.2 2.3 Hari, Johann. "Kidnapped, Raped, Married: The Extraordinary Rebellion of Ethiopia's Abducted Wives", The Independent, March 16, 2010. Retrieved on 2021-07-22. Archived from the original on 2014-08-19. 
  3. 3.0 3.1 3.2 Rosenberg, Tina. "Talking Female Circumcision Out of Existence", The New York Times, July 17, 2013. 
  4. "KMG Ethiopia". KMG Ethiopia. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2013-04-23. Iliwekwa mnamo 17 Agosti 2014. {{cite web}}: More than one of |accessdate= na |access-date= specified (help); More than one of |archivedate= na |archive-date= specified (help); More than one of |archiveurl= na |archive-url= specified (help)CS1 maint: date auto-translated (link)
  5. 5.0 5.1 "Standing up for women", The Economist, May 23, 2013. 
  6. "Fulbright Alumna Awarded King Baudouin Prize in Belgium". Bureau of Educational and Cultural Affairs. United States Department of State. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo Agosti 19, 2014. Iliwekwa mnamo Agosti 17, 2014. {{cite web}}: More than one of |accessdate= na |access-date= specified (help); More than one of |archivedate= na |archive-date= specified (help); More than one of |archiveurl= na |archive-url= specified (help)CS1 maint: date auto-translated (link)
  7. "Bogalatech Gebre (Ethiopia)" (PDF). eeas.europa.eu. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo (PDF) mnamo 28 Januari 2015. Iliwekwa mnamo 17 Agosti 2014. {{cite web}}: More than one of |accessdate= na |access-date= specified (help); More than one of |archivedate= na |archive-date= specified (help); More than one of |archiveurl= na |archive-url= specified (help)CS1 maint: date auto-translated (link)
  8. "Abducted. Raped. Married. Can Ethiopia's wives ever break free?", Abbay Media, March 17, 2010. Retrieved on 2021-07-22. Archived from the original on 2014-08-19. 
  9. Shetty, Priya. "Bogaletch Gebre: ending female genital mutilation in Ethiopia", The Lancet, June 23, 2007. 
  Makala hii kuhusu mtu huyo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Bogaletch Gebre kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.