Brisbane
Brisbane ni mji mkubwa wa tatu wa Australia na mji mkuu wa jimbo la Queensland katika kaskazini ya nchi. Idadi ya wakazi ni mnamo 1,730,000. Iko kando la mto Brisbane na mdomo wake unapita mjini.
Brisbane ulianzishwa 1824 kama makazi ya wafungwa waliopelekwa Australia kutoka Uingereza. Watu huru walikubaliwa wajenge nyumba hapa tangu 1842. Jina la mji limetokana na gavana yake ya kwanza Sir Thomas Brisbane.
Wakati wa Vita Kuu ya Pili ya Dunia Brisbane ilikuwa makao makuu ya jenerali Douglas MacArthur aliyeongoza mashambulio dhidi ya Japani.
Uchumi
haririMji ni kitovu cha biashara na uchumi kwa jimbo la Queensland. Kuna makampuni mengi ya biashara na benki pamoja na makampuni ya teknolojia ya mawasiliano na tovuti. Bandari inashughulika mazao kama nafaka na sukari pamoja na makaa.
Vyuo vikuu vya Brisbane ni maarufu kwa utafiti wa teknolojia ya kisasa.
Utalii unazidi kukua.
Mji ulikuwa mwenyeji wa michezo ya Jumuiya ya Madola ya 1982 na Maonyesho ya Dunia ya Expo '88.
Viungo vya Nje
haririMakala hii kuhusu maeneo ya Australia bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu Brisbane kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |