BrooWaha
BrooWaha ni gazeti la raia kwenye mtandao wa tarakilishi linaloripoti sana habari za eneo lake la Los Angeles. Makala zinazochapishwa kwenye tovuti yameandikwa na watumiaji wake pekee.
BrooWaha | |
---|---|
Jina la gazeti | BrooWaha |
Aina ya gazeti | Gazeti Kwenye mtandao wa tarakilishi |
Lilianzishwa | Septemba 2006 |
Eneo la kuchapishwa | Los Angeles, New York, San Francisco Atlanta Houston na Miami |
Nchi | Marekani |
Mwanzilishi | BrooWaha LLC |
Mhariri | David Cohn [1] |
Mmiliki | BrooWaha LLC |
Tovuti | http://www.broowaha.com/ |
Matoleo kadhaa ya BrooWaha yameanzishwa katika majiji makuu ya Marekani kama Los Angeles, New York, San Francisco na hivi majuzi kabisa, Atlanta, Houston na Miami. Habari zote za matoleo haya huonyeshwa katika tovuti kuu ya BrooWaha.
Tovuti hii ilionyeshwa katika gazeti la Los Angeles Times katika mwezi wa Desemba 2006.
Makala
haririWatumiaji waliosajiliwa katika tovuti ya BrooWaha huwa na ruhusa ya kuandika makala kwenye ukurasa maalum ya maandishi katika tovuti. Ukurasa huu huwezesha watumiaji kuandika makala na kuambatanisha picha na kuyawasilisha kwa wahariri. Makala, kwa kawaida, huchapishwa katika au baada ya saa 24. Licha ya kuwapa watumiaji chaguo nyingi za kuandika maandishi kwa njia mbalimbali, tovuti hiyo imepata umaarufu wa kuweza kuwa na viungo vya tovuti zingine na huonyesha video ya YouTube katika makala yao.
Wahariri
haririJukumu la wahariri wa BrooWaha ni dogo sana na hasa huwa kuthibitisha kuwa makala haya hayana ubaguzi au habari zozote zisizotakikana.. Tangu mwanzo wa mwaka wa 2008, tovuti hii imehaririwa na David Cohn [2] Archived 30 Mei 2021 at the Wayback Machine..
Maoni
haririUkurasa wa maoni ni kipengele maarufu cha BrooWaha. Majadiliano huonekana sana kati ya mwandishi wa makala na wasomaji wa makala katika kipengele hiki cha maoni. Mbali na kupigia kura makala, wasomaji huweza kupigia kura maoni ya watu wengine ili kuhimiza majadiliano mazuri.
Umaarufu
haririWatumiaji wa BrooWaha hupokea 'pointi za umaarufu' kulingana na idadi ya makala wanayoandika na umaarufu wa makala yao. Jumla ya pointi hizi inaathiri cheo chao katika shirika la gazeti hili. Makala ya watumiaji maarufu sana huonyeshwa zaidi kwenye tovuti na wao huwa na uzito zaidi wanapopiga kura kwa makala ya wengine.
Marafiki
haririWatumiaji wa BrooWaha huweza kuongeza waandishi wa habari wanaowapenda kama marafiki yao na kuarifiwa wanapoandika makala kwa kuwatumia ujumbe kwa anwani yao kwenye mtandao.
Mkahawa wa BrooWaha
haririKila toleo la BrooWaha huwa na ukurasa wa majadiliano unaoitwa BrooWaha Cafe (Mkahawa wa BrooWaha) ambapo watumaji hujadiliana kuhusu mada mbalimbali kutoka porojo hadi habari motomoto zilizofanyika.
Viungo vya nje
hariri- BrooWaha.com
- David Cohn Archived 11 Januari 2010 at the Wayback Machine.
- majadiliano na mwanziliishi Archived 12 Julai 2007 at the Wayback Machine., FishBowlLA