Bungo
Bungo wa unga (Tenebrio molitor)
Bungo wa unga (Tenebrio molitor)
Uainishaji wa kisayansi
Himaya: Animalia (Wanyama)
Faila: Arthropoda (Wanyama wenye miguu yenye viungo)
Nusufaila: Hexapoda (Wanyama wenye miguu sita)
Ngeli: Insecta (Wadudu)
Ngeli ya chini: Pterygota (Wadudu wenye mabawa)
Oda: Coleoptera (Wadudu wenye mabawa magumu)
Nusuoda: Polyphaga
Emery, 1886
Ngazi za chini

Oda za chini 4:

Bungo ni jina linalotumika kwa kawaida kwa mbawakawa wakubwa wa oda za chini Staphyliniformia, Scarabaeiformia na Elateriformia na familia za juu Tenebrionoidea na Chrysomeloidea za oda ya chini Cucujiformia, zote katika oda Coleoptera. Ili iwe rahisi inapendekezwa kuziita spishi ndogo zaidi za vikundi hivi bungo pia. Mifanano ya familia za bungo ni bungo mbawa-nusu, bungo walangozi, bungo maridadi, bungo-fyatuo, bungo-mavi, bungo wapenda-giza na bungo-lengelenge.

Spishi zilizochaguliwa za Afrika ya Mashariki

hariri

Staphyliniformia

  • Paederus sabaeus
  • Teretrius nigrescens

Scarabaeiformia

  • Homoderus gladiator
  • Scarabaeus catenatus

Elateriformia

  • Cardiophorus samburensis
  • Euphemus funerarius

Tenebrionoidea

  • Tenebrio giganteus
  • Tribolium castaneum

Chrysomeloidea

  • Conchyloctenia punctata
  • Pachnoda ephippiata