Bungo-fyatuo
Bungo-fyatuo mkubwa wa migunga (Tetralobus flabellicornis)
Bungo-fyatuo mkubwa wa migunga (Tetralobus flabellicornis)
Uainishaji wa kisayansi
Himaya: Animalia (Wanyama)
Faila: Arthropoda (Wanyama wenye miguu yenye viungo)
Nusufaila: Hexapoda (Wanyama wenye miguu sita)
Ngeli: Insecta (Wadudu)
Ngeli ya chini: Pterygota (Wadudu wenye mabawa)
Oda: Coleoptera (Wadudu wenye mabawa magumu)
Nusuoda: Polyphaga
Familia ya juu: Elateroidea
Familia: Elateridae
Leach, 1815
Ngazi za chini

Nusufamilia 19, 4 katika Afrika ya Mashariki:

Bungo-fyatuko ni mbawakawa wa familia Elateridae katika nusuoda Polyphaga ya oda Coleoptera walio na njia ya kurudi kwa miguu yao baada ya kutua chali kwa kujisukuma angani ambapo hujaribu kugeuka na kutua kwa miguu yao. Lava wao huishi ardhini na kuitwa nyunguwaya ([[w:wireworm|wireworms) kwa sababu ya umbo lao jembamba na refu na ushupavu wao kulinganisha na lava wa bungo wengine. Kuna spishi 9300 duniani kote[1]; idadi ya spishi za Afrika ya Mashariki haijahesabiwa.

Maelezo

hariri
 
Picha ya upande wa chini wa kichwa na toraksi za bungo-fyatuo ambayo inaoyesha kulabu na tundu ya mfumo wa ufyataji. Inaonyesha pia vipapasio na miguu ndani ya mifuo yao.

Bungo hao wana urefu wa sm 0.2-7 lakini wengi sana ni chini ya sm 2. Baadhi yao wana rangi kali lakini wengine ni weusi au kahawia bila mabaka. Kwa kawaida urefu wa vipapasio ni nusu ya ule wa mwili na vinaweza kukunjwa katika mifuo kwenye upande wa chini wa kichwa. Mifuo ingine iko kwenye pronoto ili kupokea miguu.

Kulabu inatokeza upande wa chini wa pingili ya kwanza ya pronoto ambaye inawafikia tundu kwenye pingili ya pili. Ikiwa bungo anapolala chali au kutishwa na adui, anaingiza kulabu katika tundu hili kwa kupinda pronoto. Kisha bungo huvuta kulabu hadi inafyatua nje huku ikitokeza kidoko kinachosikika. Kwa sababu ya hii pingili ya kwanza inapiga chini kwa nguvu sana kwamba bungo husukumwa angani ambapo anajaribu kugeuka na kutua kwa miguu yake[2].

Bungo-fyatuo wanaweza kuruka angani, lakini hawawezi kuruka kutoka ardhi au sehemu nyingine bapa. Lazima wapande juu ya kitu wima, kama mti, kikingi n.k., kabla ya kufungua mabawa.

Lava ni warefu na wembamba wenye kutikulo ngumu kiasi. Kwa hivyo mwili umeshupaa kama waya na kwa sababu ya hii huitwa nyunguwaya. Kwa kawaida wana rangi ya manjano au ya machungwa isiyokolea.

Biolojia na ekolojia

hariri

Kwa kawaida bungo-fyatuo hukiakia usiku na kwa hivyo hawaonekani mara nyingi, ingawa, usiku wa joto, huvutiwa na mwanga na wanaweza kuingia ndani ya nyumba. Wanakula sehemu za mimea, lakini spishi kadhaa tu zina umuhimu wa kiuchumi. Ingawa nyunguwaya wa spishi fulani hukamilisha ukuaji wao katika mwaka mmoja (k.m. Monocrepidius), wengi wao hutumia miaka mitatu au minne kwenye udongo. Nyunguwaya kawaida hula viumbe waliokufa, lakini spishi kadhaa hula mizizi ya mimea na wanaweza kuwa wadudu waharibifu wa kilimo. Wengine ni mbuai wamilifu wa lava wa wadudu wengine.

Usumbivu

hariri

Kwa kula mizizi ya mimea, nyunguwaya mara nyingi husababisha uharibifu wa mazao ya kilimo kama vile viazi, sitroberi, mahindi na ngano[3][4], lakini pia kwa nyasi, kama vile katika viwanja vya gofu. Tabia za chini ya ardhi za nyunguwaya, kama uwezo wao wa kupata chakula kwa haraka kwa kufuata viwango vya juu vya kaboni dioksidi zinazozalishwa na dutu za mimea kwenye udongo[5], na uwezo wao wa ajabu wa kupona kutokana na magonjwa yanayosababishwa na kuathiriwa na viuawadudu (wakati mwingine baada ya miezi mingi)[6], zinaifanya ngumu kuwaangamiza mara tu wameanza kushambulia mazao. Nyunguwaya wanaweza kupita kwa urahisi kwenye udongo kwa sababu ya umbo lao na mwelekeo wao wa kufuata mashimo yaliyokuwepo awali[7], na wanaweza kusafiri kutoka mmea hadi mmea, hivyo basi kuumiza mizizi ya mimea mingi ndani ya muda mfupi. Mbinu za kudhibiti waharibifu ni pamoja na mzunguko wa mazao na kusafisha ardhi ya wadudu kabla ya kupanda.

Spishi zilizochaguliwa za Afrika ya Mashariki

hariri
  • Cryptalaus sp.
  • Euphemus funerarius
  • Hemicrepidius nemnonius
  • Melanotus sp.
  • Orthostethus sp.
  • Tetralobus flabellicornis

Marejeo

hariri
  1. Schneider, M. C.; na wenz. (2006). "Evolutionary chromosomal differentiation among four species of Conoderus Eschscholtz, 1829 (Coleoptera, Elateridae, Agrypninae, Conoderini) detected by standard staining, C-banding, silver nitrate impregnation, and CMA3/DA/DAPI staining". Genetica. 128 (1–3): 333–346. doi:10.1007/s10709-006-7101-5. PMID 17028962. S2CID 1901849.
  2. Kigezo:Cite AV mediaKigezo:Cbignore
  3. R. S. Vernon; W. van Herk; J. Tolman; H. Ortiz Saavedra; M. Clodius; B. Gage (2008). "Transitional sublethal and lethal effects of insecticides after dermal exposures to five economic species of wireworms (Coleoptera: Elateridae)". Journal of Economic Entomology. 101 (2): 365–374. doi:10.1603/0022-0493(2008)101[365:TSALEO]2.0.CO;2. PMID 18459400.
  4. William E. Parker; Julia J. Howard (2001). "The biology and management of wireworms (Agriotes spp.) on potato with particular reference to the U.K." Agricultural and Forest Entomology. 3 (2): 85–98. doi:10.1046/j.1461-9563.2001.00094.x.
  5. J. F. Doane; Y. W. Lee; N. D. Westcott; J. Klingler (1975). "The orientation response of Ctenicera destructor and other wireworms (Coleoptera: Elateridae) to germinating grain and to carbon dioxide". Canadian Entomologist. 107 (12): 1233–1252. doi:10.4039/Ent1071233-12.
  6. W. G. van Herk; R. S. Vernon; J. H. Tolman; H. Ortiz Saavedra (2008). "Mortality of a wireworm, Agriotes obscurus (Coleoptera: Elateridae), after topical application of various insecticides". Journal of Economic Entomology. 101 (2): 375–383. doi:10.1603/0022-0493(2008)101[375:moawao]2.0.co;2. PMID 18459401.
  7. Willem G. van Herk; Robert S. Vernon (2007). "Soil bioassay for studying behavioral responses of wireworms (Coleoptera: Elateridae) to inecticide-treated wheat seed". Environmental Entomology. 36 (6): 1441–1449. doi:10.1603/0046-225X(2007)36[1441:SBFSBR]2.0.CO;2. PMID 18284772.