Calcipotriol
Calcipotriol, pia inajulikana kama calcipotriene, ni dawa inayotumika kutibu hali ya seli za ngozi kujijenga na kutengeneza gamba na mabaka makavu yanayowasha (psoriasis).[1] Dawa hii inatumika kwa ngozi na inapatikana pia pamoja na betamethasone (dawa inayotumika kutibu hali mbalimbali za uvimbe na mzio).[1]
Madhara yake ya kawaida ni pamoja na kuhisi usumbufu kwenye ngozi, kuwasha na psoriasis (gamba na mabaka makavu kwenye ngozi) kali sana.[1] Madhara yake mengine yanaweza kujumuisha kuongezeka kwa unyeti kwa mionzi ya UV na kalsiamu nyingi.[1] Usalama wa matumizi yake katika ujauzito hauko wazi.[1] Dawa hii ni katika vitu vinavyotokana (derivative) na calcitriol, aina ya vitamini D.[2]
Calcipotriol ilipewa hati miliki katika mwaka wa 1985 na kuidhinishwa kwa ajili ya matumizi ya kimatibabu mwaka wa 1991.[3] Iko kwenye Orodha ya Dawa Muhimu ya Shirika la Afya Ulimwenguni[4] na inapatikana kama dawa ya kawaida.[5] Nchini Marekani, gramu 60 hugharimu takriban dola 70 za Marekani kufikia mwaka wa 2021.[5]
Marejeo
hariri- ↑ 1.0 1.1 1.2 1.3 1.4 "Calcipotriene Monograph for Professionals". Drugs.com (kwa Kiingereza). Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 26 Julai 2017. Iliwekwa mnamo 29 Desemba 2021.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ "Calcipotriol". SPS - Specialist Pharmacy Service. 28 Aprili 2015. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 11 Oktoba 2021. Iliwekwa mnamo 29 Desemba 2021.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ Fischer, Jnos; Ganellin, C. Robin (2006). Analogue-based Drug Discovery (kwa Kiingereza). John Wiley & Sons. uk. 452. ISBN 9783527607495. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2021-01-22. Iliwekwa mnamo 2021-03-03.
- ↑ World Health Organization (2023). The selection and use of essential medicines 2023: web annex A: World Health Organization model list of essential medicines: 23rd list (2023). Geneva: World Health Organization. hdl:10665/371090. WHO/MHP/HPS/EML/2023.02.
- ↑ 5.0 5.1 "Calcipotriene Prices, Coupons & Savings Tips - GoodRx". GoodRx. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 25 Oktoba 2016. Iliwekwa mnamo 29 Desemba 2021.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link)
Makala hii kuhusu mambo ya tiba bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Calcipotriol kama sababu yake au mahusiano yake na mada nyingine? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |