Chanjo ya homa ya uti wa mgongo inayosababishwa na kuvu
Chanjo ya homa ya uti wa mgongo inayosababishwa na kuvu hurejelea chanjo yoyote ambayo hutumika kuzuia maambukizi ya Neisseria meningitidis.[1] Toleo mbalimbali ni faafu dhidi ya baadhi ya au aina zote zifuatazo za homa ya uti wa mgongo inayosababishwa na kuvu: A, C, W135, na Y. Chanjo hizo hufanya kazi kwa kati ya 85% na 100% kwa angalau miaka miwili.[1] Husababisha upungufu wa homa ya uti wa mgongo na sepsis miongoni mwa idadi ya watu wanazozitumia sana.[2][3] Hutolewa ama kwa kudungwa sindano kwenye misuli au chini ya ngozi tu.[1]
Shirika la Afya Duniani linapendekeza kwamba nchi zilizo na kiwango cha wastani au cha juu cha ugonjwa huo au na maambukizi ya mara kwa mara zinafaa kutoa chanjo kila mara.[1][4] Katika nchi zenye hatari ya chini ya ugonjwa huo, wanapendekeza kwamba makundi yenye hatari ya juu yanafaa kupewa chanjo.[1] Katika maeneo yenye hatari ya homa ya uti wa mgongo, juhudi za kuwapa chanjo watu wote kati ya umri wa mwaka mmoja na miaka thelathini wenye homa ya uti wa mgongo A zinaendelea.[4] Katika Kanada na Marekani chanjo zinazofanya kazi kwa aina zote nne zinapendekezwa mara kwa mara kwa vijana na wengine walio kwenye hatari ya juu.[1] Zinahitajika pia kwa watu wanaosafiri kwenda Mecca kwa ajili ya Hajj.[1]
Usalama kwa ujumla ni nzuri. Wengine huwa na uchungu na wekundu katika sehemu zilizodungwa sindano.[1] Matumizi wakati wa ujauzito ni salama.[4] Athari kali za mzio hutokea kwa chini ya kiwango kimoja kwa viwango milioni moja.[1]
Chanjo ya kwanza ya homa ya uti wa mgongo inayosababishwa na kuvu ilibuniwa miaka ya 1970.[5] Ipo kwenye Orodha ya Dawa Muhimu ya Shirika La Afya Duniani, dawa muhimu zaidi inayohitajika kwenye mfumo wa afya.[6] Bei ya ununuzi wa jumla ni kati ya dola 3.23 na dola 10.77 kwa kila kipimo mnamo 2014.[7] Gharama yake Marekani ni kati ya dola 100 na 200.[8]
Tanbihi
hariri- ↑ 1.0 1.1 1.2 1.3 1.4 1.5 1.6 1.7 1.8 "Meningococcal vaccines: WHO position paper" (PDF). Weekly epidemiological record. 47 (86): 521-540. Nov 2011. PMID 22128384.
- ↑ Patel, M; Lee, CK (25 January 2005). "Polysaccharide vaccines for preventing serogroup A meningococcal meningitis". The Cochrane Database of Systematic Reviews (1): CD001093. PMID 15674874.
- ↑ Conterno, LO; Silva Filho, CR; Rüggeberg, JU; Heath, PT (19 July 2006). "Conjugate vaccines for preventing meningococcal C meningitis and septicaemia". The Cochrane Database of Systematic Reviews (3): CD001834. PMID 16855979.
- ↑ 4.0 4.1 4.2 "Meningococcal A conjugate vaccine: updated guidance, February 2015" (PDF). Weekly epidemiological record. 8 (90): 57-68. 20 Feb 2015. PMID 25702330.
- ↑ Barrett, Alan D.T. (2015). Vaccinology : an essential guide. p. 168. ISBN 9780470656167.
- ↑ "WHO Model List of EssentialMedicines" (PDF). World Health Organization. October 2013. Retrieved 22 April 2014.
- ↑ "Vaccine, Meningococcal Ilihifadhiwa 10 Mei 2017 kwenye Wayback Machine.". International Drug Price Indicator Guide. Retrieved 6 December 2015.
- ↑ Hamilton, Richart (2015). Tarascon Pocket Pharmacopoeia 2015 Deluxe Lab-Coat Edition. Jones & Bartlett Learning. p. 315. ISBN 9781284057560.
Makala hii kuhusu mambo ya tiba bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Chanjo ya homa ya uti wa mgongo inayosababishwa na kuvu kama sababu yake au mahusiano yake na mada nyingine? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |