Chantal Biya (amezaliwa 1970) ni First Lady wa Kamerun. Alizaliwa Dimako, Mkoa wa Mashariki, na mtaalam wa kigeni wa Kifaransa Georges Vigouroux na mshindi wa tuzo la urembo la Miss Doumé, Rosette Ndongo Mengolo. Chantal Biya ujanani aliishi Yaoundé. [1]

Chantal Biya na Laura Bush baada ya kahawa katika White House, 21 Machi 2003

Aliolewa na Rais Paul Biya mnamo tarehe 23 Aprili 1994, baada ya mke wake wa kwanza, Jeanne-Irene Biya, kuaga dunia mwakani 1992. Chantal Biya ameanzisha mashirika hisani kadhaa. Miongoni mwao ni African Synergy, ambalo huendeleza mipango mbalimbali ya VVU / UKIMWI, na Chantal Biya Foundation (Kifaransa Fondation Chantal Biya). Aliandaa Kongamano la First Ladies la kwanza mjini Yaoundé wakati wa kongamano la Umoja wa Afrika[2] la 1996 Jeunesse Active pour Chantal Biya ni sehemu ya Cameroon People Democratic Movement cha mumewe.[3]

Miongoni mwa wanawake wa Kamerun, Biya ni maarufu kwa sababu ya mitindo ya nywele. Staili yake ya kawaida inaitwa the banana, na hutumiwa kwa hafla rasmi. [4] Biya ameeneza mitindo mingine; pamoja, inayojulikana kama the Chantal Biya. [5] Pia anajulikana kwa sababu ya nguo zake. Baadhi ya wasanifu anaopenda zaidi wanajumuisha walio bora zaidi Ulaya kama vile Chanel au Dior. [6]

Grand Prix Chantal Biya ni mashindano wa baiskeli ya wataalam katika barabara ya UCI Afrika Tour. Mamake Chantal, Rosette Marie Mboutchouang, alichaguliwa Meya wa Bangou kufuatia uchaguzi wa manispaa mnamo Julai 2007.

Tanbihi

hariri
  1. Morikang.
  2. Ibrahim 17.
  3. Ngwane 17.
  4. Nyamnjoh et al. 113.
  5. Nyamnjoh et al. 117.
  6. http://www.elmundo.es/yodona/albumes/2009/03/20/chantalbiya_style/index.html

Marejeo

hariri

Viungo vya nje

hariri