Yaunde

(Elekezwa kutoka Yaoundé)

Yaoundé ni mji mkuu na mji mkubwa wa pili nchini Kamerun baada ya Douala. Ina wakazi milioni 1,3.

Jiji la Yaounde
Nchi Kamerun
Mahali pa Yaoundé katika Kamerun
Yaoundé

JiografiaEdit

Mji uko kwenye kimo cha 730 m juu ya UB katika vilima vya Kamerun ya magharibi takriban 160 km kutoka mwambao wa Atlantiki. Hali ya hewa ni ya kitropiki; halijoto ina wastani ya 23.3 C°. Mvua hunyesha Septemba / Oktoba na Aprili / Mei.

HistoriaEdit

Yaounde ilianzishwa mwaka 1888 BK na wanfanya biashara Wajerumani. Baada ya Vita Kuu ya Kwanza ya Dunia na mgawanyo wa nchi ikawa sehemu ya Kamerun ya Kifaransa na mji mkuu wa koloni kuanzia mwaka 1922. Wakati wa uhuru mwaka 1961 ilikuwa mji kuu wa Kamerun yote pamoja na sehemu zilizokuwa chini ya Uingereza.

UchumiEdit

Yaounde ni kitovu cha usafiri na mawasiliano ya nchi. Kuna viwanda vya tumbako, vyakula, vioo na ubao. Yaounde ni kitovu cha biashara kwa ajili ya kilimo cha kahawa, kakao, nguta na raba katika mazingira ya mji. Kuna pia migodi ya dhahabu na metali ya titani.

Wamezaliwa YaoundeEdit

  • Roger Milla (20 februari 1952) mcheza mpira wa miguu
  • Franck Songo'o (14 mei 1987) mcheza mpira wa miguu

Viungo vya njeEdit