Chedieli Yohane Mgonja

Chedieli Yohane Mgonja (1934-2009) alikuwa mwanasiasa wa Tanzania.

HISTORIA YA CHEDIELI YOHANE MGONJAEdit

KuzaliwaEdit

kuzaliwa 31 Desemba 1934, Vudee Same-Magharibi(Wilaya ya Pare)

ElimuEdit

shule ya msingi Vudee, sekondari Ilboru na Tabora.

1959 ---Chuo Kikuu Makerere.

1960 ---Bwana Shauri Tanga.

1961 --- miongoni mwa Watanganyika sita waliotunukiwa zawadi kwa kushiriki ktk shindano la utenzi wa wimbo wa taifa wa Tanganyika.

1961 --- 62 Chuo Kikuu Cambridge UK -- kozi ya utawala na Diplomasia. Wengine katika kozi hiyo ni walioapata kuwa mabalozi George Nhigula,John Malecela, Bernard Mulokozi, Raphael Lukindo, Akili Daniel.

1962 --- Ubalozi wa Tanganyika New York.

1964 --- kuomba kurudi nyumbani kwa nia ya kugombea Ubunge.

1965 --- kupigania ubunge wilaya ya Pare vs Naibu Waziri na katibu mwenezi wa Tanu Elias Kisenge.

1965 --- 67 Mbunge wilaya ya Pare, Waziri wa Maendeleo na Utamaduni. rekodi ya kuwa waziri kijana kuliko wote Tanzania.

1967 -- 68 Waziri wa Nchi Ofisi ya Raisi ( Mambo ya Nje ). Waziri wa kwanza kujiunga na mafunzo ya JKT. Baadaye kuendelea na mafunzo ya mgambo. Waziri aliyetoa tamko la serikali ya Tanzania kuitambua Jamhuri ya watu wa Biafra.

1968 -- 72 Waziri wa Elimu. Mabadiliko makubwa katika mfumo wetu wa elimu yalifanyika kipindi cha uongozi wake.

1972 -- 75 Mkuu wa Mkoa na Katibu wa Chama Mtwara. Ni uteuzi pekee ambao Mwalimu alimjulisha kabla haujatangazwa. Ilikuwa ni kipindi cha madaraka mikoani na vita ya ukombozi ya Msumbiji. Mkoa wa Mtwara kushika nafasi ya pili, ukifuatia Dar es Salaam, katika kuchangia vita vya ukombozi.

1977 -- Mkuu wa Mkoa na Katibu wa Chama Tabora.

1977 -- 1980 Waziri wa Utamaduni, Vijana, na Michezo. Tanzania kukataa shinikizo la Marekani kususia michezo ya Olimpia mjini Moscow. Ujumbe wa Marekani uliletwa na Mohamed Ali.

1980 -- 1982 kushinda Ubunge. Kushinda kesi dhidi yake mahakama Kuu Arusha. Kuvuliwa Ubunge na mahakama ya Rufaa Tanzania.

1984 -- kuteuliwa na Raisi Mkuu wa Mkoa Shinyanga.

1985 -- 95 Mbunge Wilaya ya Same: vs Jonas Manento (85) vs. Dr.Kivurunya Mtera (90).

SIASAEdit

Alikuwa Waziri wa Elimu, Habari na Michezo, na Waziri wa nchi mambo ya nje. Aliwahi kuwa Mkuu wa mkoa wa Mtwara na Tabora. Aliingia kwenye siasa mwaka 1965, akiwa Mbunge wa Upare/Same na mwaka huo huo akateuliwa kuwa waziri wa utamaduni, siasa na michezo.

Mgonja alikuwa kwenye siasa mpaka mwaka 1995, ambapo wakati wote alikuwa akiliwakilisha wilaya ya Same.

Mgonja aliongoza wizara mbalimbali katika Serikali ya awamu ya kwanza.

==Mafanikio ya Mgonja Katika Wilaya yake ya Same ==. Kwa upande wa Elimu alisisitiza ujenzi wa shule za msingi kila kata katika jimbo lake la same. Ndio maana wakati wake wasomi wengi walitoka Upareni na Kilimanjaro kwa ujumla.

Ujenzi wa Miundo Mbinu: Wilaya ya Same ina milima mingi sana, lakini pamoja na milima hiyo wananchi wa Same chini ya uongozi wa ndugu Mgonja waliweza kuchonga bara bara kwenye miteremko hiyo mikali, kwa kutumia falsafa ambayo Wapare wanaita "MSARAGAMBO" ambapo Mwalimu Nyerere alipotembelea Vudee na kuona kazi nzuri ya ujenzi wa barabara iliyofanywa na wananchi wa Same hasa Vudee aliwaita "Wachina" wa Tanzania.

KESI YA UCHAGUZI YA CHEDIELI YOHANE MGONJAEdit

Katika uchaguzi wa mwaka 1980 Mgonja alishitakiwa kwenye kesi ya uchaguzi kuwa aliiba kura za uchaguzi (election irregularities) na kwa hiyo ushindi wake wa ubunge hakuwa halali.

1980 -- 1982 kushinda Ubunge. Kushinda kesi dhidi yake mahakama Kuu Arusha. Kuvuliwa Ubunge na mahakama ya Rufaa Tanzania.Mahakama ya rufaa ya Tanzania ilimhukumu Mgonja kutoshiriki siasa/uchaguzi kwa kipindi cha miaka 10 katika kesi ya uchaguzi ya miaka ya 80.

Mwaka 1983 Kuteuliwa na Mwalimu J.K.Nyerere kuwa Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga. Mwalimu akamteua Mgonja kuwa mkuu wa mkoa wa Shinyanga kabla ya kumalizika adhabu yake. Mwanasheria Mkuu wa wakati ule Joseph Sinde Warioba alimshauri mwalimu kuwa suala hilo lingeleta mgogoro wa Kikatiba bungeni. Kwa hiyo Waziri Mkuu Sokoine alimshauri Mwalimu na kutengua uteuzi wake.

Kabla Mwalimu Nyerere hajaondoka madarakani alimpunguzia Mgonja adhabu yake. Mgonja aligombea ubunge wa Same katika uchaguzi wa mwaka 1985, wananchi wa Same walimpa ushindi Mgonja. Katika uchaguzi wa mwaka 1990, wananchi wa Same, walimrudisha bungeni tena kipenzi chao Chedieli Yohane Mgonja "Kaghembe".

Na mwaka 1995 ukawa mwisho wake wa kushiriki siasa.

KUFARIKIEdit

Alifariki tarehe 30 Januari 2009, kwa ugonjwa wa kisukari na shinikizo la damu jijini Dar es salaam. Mke wake anaitwa Lilian Mgonja na bado yuko hai kijijini kwake Vudee Same Magharibi. Mgonja alikuwa ni mkazi wa kijiji cha Vudee Same Kilimanjaro.

MWANDISHI WA KITABUEdit

Ameandika Kitabu kinachoitwa "JOHARI YA MAISHA YANGU".