Chekechea

Chekechea, maana yake ni kitu kidogo, hivyo pia watoto wadogo.

Siku ya kwanza ya mwaka wa masomo kwa watoto wa chekechea na wanafunzi wapya wa shule ya msingi, Nishapur, Iran.

Neno hilohilo linatumika pia kwa vituo vya kuwalea (kwa Kiingereza "kindergarten", yaani "bustani ya watoto"). Ndiyo hatua ya kwanza kuelekea elimu rasmi.

Watoto katika vituo hivyo wanajifunza kupitia michezo mbalimbali.

Umri wao kwa kawaida ni kati ya miaka 3 na 7.