Chuo Kikuu cha Mansoura

Chuo Kikuu cha Mansoura kilianzishwa mwaka 1972 katika mji wa Mansoura, Misri. Kiko katikati ya Delta ya Nile. Ni mojawapo ya vyuo vikuu vikubwa zaidi nchini Misri na kimechangia sana katika maisha ya kitamaduni na kisayansi huko Mansoura na Misri.

Gāmaʿat al-Mansoura

Historia

hariri

Fakulti ya Tiba ilianzishwa mwaka 1962 kama tawi la Chuo Kikuu cha Cairo.[1] Mnamo 1972, amri ya rais ilitangaza kuanzishwa kwa chuo kikuu hicho kwa jina "Chuo Kikuu cha Delta ya Mashariki". Jina lake lilibadilishwa kuwa Chuo Kikuu cha Mansoura mnamo 1973.

Mnamo 2018, Mansourasaurus, jenasi ya dinosaur wa mimea wa lithostrotian sauropod,[2] iligunduliwa na timu chini ya mwanasayansi wa masalia ya kale wa Chuo Kikuu cha Mansoura, Hesham Sallam, na ilipewa jina kwa heshima ya chuo kikuu hicho.[3]

Tanbihi

hariri
  Makala hii kuhusu mambo ya elimu bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Chuo Kikuu cha Mansoura kama historia yake, uenezi au maendeleo yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.