Sayansi

biashara ya kimfumo ambayo hujenga na kupanga maarifa, na seti ya maarifa inayotolewa na biashara hii
(Elekezwa kutoka Kisayansi)

Sayansi ni maarifa yanayopatikana kwa kufanya vitendo, kutazama na kujaribu kweli ambazo zimebainishwa hazijathibitishwa.[2]

Galileo Galilei, baba wa sayansi ya kisasa.[1]: Vol. 24, No. 1, p. 36 

Mara nyingi Galileo Galilei anahesabiwa kuwa baba wa sayansi ya kisasa.

Aina za sayansi

 
Mtu aliyerushwa hadi angani. Kufikia katikati ya karne ya 20 binadamu ameweza kukua kisayansi na hivyo kuvumbua teknolojia zilizomwezesha kuruka na kuelea katika anga la juu kabisa la Dunia kwa mara ya kwanza na kuchunguza anga-nje.

Kuna sayansi mbalimbali ambazo huainishwa katika makundi yafuatayo:

Sayansi Asili k.m.

Sayansi Umbile k.m.

Sayansi Jamii k.m.

Sayansi Tumizi k.m.

Pia, kuna sayansi zinazohusu mada maalumu mbalimbali:

Mbinu za kisayansi

 
Charles Darwin mwaka 1854, alipokuwa anatunga kitabu chake "On the Origin of Species".

Msingi wa sayansi ni vitendo. Vitendo vya kisayansi vina njia zake zinazotumika kuthibitisha kweli fulani.

Namna ya kueleza jambo kisayansi huchimbuka toka nadharia ama udhanifu. Halafu, ili kweli ikubalike, hutoka kwenye udhanifu na kwa kupitia majaribio rasmi, hutengeneza dhana kamili ama nadharia kama ni shauri la kueleza mwenendo na tabia.

Hivyo, asili ya njia ya kisayansi ni mtazamo unaokwenda sambamba na vitendo vinavyochunguzwa. Kutoka mitazamo wanasayansi wanaunda nadharia. Baadaye wanaangalia kama bashiri za nadharia ni kweli. Zisipokuwa kweli watakanusha nadharia hiyo. Ikionekana kwamba mara nyingi sana nadharia ilibashiri ukweli, na haijakosea, itakuwa nadharia inayokubalika.

Sura ya kisayansi

Mara chache, maarifa yatokanayo na sayansi yanaweza kupinga hali ya kawaida. Kwa mfano nadharia ya atomu inasema kwamba katika jiwe (maada yabisi) kuna uvungu (dutu tupu), na kwamba atomi zinacheza katika nafasi ndogo katika jiwe ukifananisha na maada kimiminika. Lakini kwa nadharia hii tunaweza kueleza mambo mengi, hata kwa nini tunaweza kusema kwamba jiwe halina uvungu.

Historia

 
Aristotle (384 KK322 KK) alichangia ukuaji wa sayansi.

Sura ya kiutamaduni

Sayansi iliaanza kama udadisi wa mtu mmojammoja; lakini kadiri maarifa yanavyopanuka, inakuwa vigumu kwa mtu mmoja kufanya mchango wa kujitenga. Hivyo jumuiya zimebeba kusudi ambalo hapo mwanzo lilionekana kama ni shauku la mtu mmojammoja kama awali.

Hii hufanya mkururo wa ugunduzi ama uvumbuzi kuwa sehemu ya historia ya sayansi. Majina na sifa hutajwa sambamba na shauri la aliyepelekea.

Sayansi na jamii huenda pamoja katika kuleta mabadiliko, kwa kuwa mabadiliko huletwa na watu wenyewe.

Sayansi na siasa za dunia

 
Picha ya dunia ikionyesha kutokea kwa mabara tangu kugawanyika kwa Pangea mpaka hivi leo.

Katika dunia hii ya leo, maendeleo ya watu hujidhihirisha sana kutokana na jinsi jamii husika ilivyopiga teke katika uwanja huu.

Ingawaje haibainishwi wazi miongoni mwa sura ya mambo ya kidunia, sayansi kwa kweli ni nguvu inayoweza kubadili maisha ya watu kwa wema; lakini katika kilele chake cha mafanikio, vyombo vyenye nguvu za mamlaka na fedha hushikilia baadhi ya matunda yake katika hali ya kibiashara na kiutawala zaidi.

Sayansi na maendeleo

 
Mambo mbalimbali ya kikemikali yaliyosomwa na Michael Faraday na kuripotiwa katika kitabu Historia ya kikemikali ya mshumaa mwaka 1861.

Wapo watu pia ambao hutumia sayansi kujaribu kuboresha maisha ya watu wote kwa ujumla. Hivyo sayansi haibakii tu mikononi mwa wenye kushika dau kimifumo, bali changamoto ya wote wenye kutaka kuleta maendeleo ya ujumla.

Hivyo roho ya uchunguzi ndiyo iliyoleta kuzaliwa, kukua na kutapakaa kwa sayansi.

Tazama pia

Tanbihi

  1. "Galileo and the Birth of Modern Science". American Heritage of Invention and Technology. 24.
  2. Ufafanuzi katika Kamusi ya Kiswahili Sanifu: "sayansi /sajansi/ nm (-) [i—] elimu inayotokana na uchunguzi, majaribio, vipimo na kuthibitishwa kwa muda uliopo. " Ufafanuzi katika Kamusi Kuu: "sayansi - tawi la maarifa linalohusu nadharia, vipimo, uchunguzi wa hatua kwa hatua na uthibitishaji wa kuwepo au kutokuwepo kwa kitu au jambo katika hali halisi "
  Makala hii kuhusu mambo ya sayansi bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Sayansi kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.