Chuo cha Mt. Petro, Auckland
Chuo cha Mtakatifu Petro, Auckland (kwa Kiingereza: St Peter's College, Auckland) ni shule ya sekondari ya Kikatoliki kwa wavulana tu iliyoko mjini Auckland, Nyuzilandi. Ni shule kubwa kabisa ya Kikatoliki nchini Nyuzilandi.
Ilianzishwa mnamo 1939 na shirika la Christian Brothers (Ndugu wa Kikristo), lakini tangu mwaka wa 2008 ni chini ya serikali na imeruhusiwa kuwa na idadi ya wanafunzi isiyozidi 1200. Kufuatana na orodha ya wanafunzi ya tarehe 26 Agosti 2009, kulikuwa na wanafunzi 1127, na 52 ni wa kimataifa. Watu mashuhuri waliohitimu shule hiyo ni kama Bwana Michael Fay (mfanyabiashara na mwanariadha wa yoti) na Sam Hunt (mshairi).
Kitaaluma, shule inatoa masomo yanayolengea National Certificate of Educational Achievement (Cheti cha Kitaifa cha Kuhitimu Katika Masomo) na Cambridge International Examinations (Mitihani ya Kitaifa ya Cambridge).
Habari mbalimbali za shule
haririWito: Kupenda na Kuhudumia (kwa Kiingereza To Love and To Serve; kwa Kilatini Amare et Servire)
Aina: Shule ya Sekondari ya Kikatholiki kwa Wavulana (Darasa 7-13)
Mkuu wa shule: K.F. Fouhy
Anwani: 23 Mountain Rd, Epsom, Auckland, New Zealand