Nyuzilandi
Nyuzilandi (kwa Kiingereza New Zealand kwa Kimaori: Aotearoa) ni nchi ya visiwani katika Pasifiki takriban km 1,500 upande wa mashariki-kusini wa Australia. Inajumuisha maeneo mawili makuu ya ardhi—Kisiwa cha Kaskazini (Te Ika-a-Māui) na Kisiwa cha Kusini (Te Waipounamu). Ni nchi ya visiwa ya sita kwa ukubwa kwa eneo na iko mashariki ya Australia kupitia Bahari ya Tasmania na kusini mwa visiwa vya New Caledonia, Fiji, na Tonga.
New Zealand (Kiingereza) Aotearoa (Kimaori) |
|||
![]() |
![]() |
||
Wimbo wa taifa God Defend New Zealand (Mungu Ilinde New Zealand) |
|||
Eneo la Nyuzilandi |
|||
Mji Mkuu | Wellington | ||
---|---|---|---|
Jiji kubwa | Auckland | ||
Lugha Rasmi | |||
Kabila |
|
||
Aina ya Serikali | Ufalme wa kikatiba | ||
Gavana Mkuu | Cindy Kiro | ||
Waziri Mkuu | Chris Hipkins | ||
Ukubwa wa eneo | |||
Jumla | 268,680 km² | ||
Idadi ya watu | |||
Kadirio (2021) | 5,132,870 | ||
Sensa (2018) | 4,699,755 | ||
Msongamano | 19.1 /km² | ||
Pato la taifa PPP (2024) | |||
Jumla | ![]() |
||
Capita | ![]() | ||
Pato la taifa (2024) | |||
Jumla | ![]() |
||
Capita | ![]() |
||
Kiashiria cha maendeleo ya watu (2019) | 0.931 (ya 14) Maendeleo ya Juu Sana |
||
Kiashiria cha ukosefu wa usawa (2022) |
30
Ukosefu wa usawa wa kati |
||
Sarafu | Dola ya Nyuzilandi | ||
Eneo la saa | (UTC +12) NZST | ||
Nambari ya mwito | +64 | ||
Jina la kikoa | .nz |
Eneo lake linaundwa na visiwa viwili vikubwa: Kisiwa cha Kaskazini (North Island au Te Ika-a-Māui) na Kisiwa cha Kusini (South Island au Te Waipounamu) na vingine 600 vidogo.
Jiografia
haririMiji
hariri- Wellington ni mji mkuu wa Nyuzilandi.
- Auckland ndio mji mkubwa visiwani.
Miji mingine ni:
Watu
haririIdadi ya wakazi ni 4,690,000. Wengi wao (74%) bado wana asili ya Ulaya, ingawa asilimia yao inazidi kupungua. Wakazi asilia ni Wamaori waliotokea Polinesia na kuhamia visiwa hivyo kati ya miaka 1250-1300 BK; kwa sasa ni 14.9% ya wakazi wote. Wengine wana asili ya Asia (11.8%) na ya visiwa vya Pasifiki (7.4%).
Lugha rasmi ni Kiingereza, Kimaori na Lugha ya Ishara ya Nyuzilandi (kwa Kiingereza: New Zealand Sign Language au NZSL).
Upande wa dini, 49% ni Wakristo wa madhehebu mbalimbali, kuanzia Kanisa Katoliki (12.6%), Anglikana (11.8%) na Wapresbiteri (8.5%). Idadi ya wasio na dini inazidi kupanda na imeshafikia 38.55%, mbali ya 12.27% wasiojibu swali kuhusu hilo. Kuna Mabanyani (2.1%), Wabuddha (1.5%), Waislamu (1.2%), Singasinga (0.5%)
Tazama pia
haririViungo vya nje
hariri- (Kiingereza) Tovuti rasmi Ilihifadhiwa 13 Agosti 2007 kwenye Wayback Machine.
Nchi_na maeneo ya Australia na Pasifiki |
Australia | Fiji | Guam | Hawaii | Kaledonia Mpya | Kiribati | Kisiwa cha Pasaka | Mikronesia | Nauru | Nyuzilandi | Niue | Pitcairn | Polinesia ya Kifaransa | Palau | Papua Guinea Mpya | Samoa | Samoa ya Marekani | Visiwa vya Cook | Visiwa vya Mariana ya Kaskazini | Visiwa vya Marshall | Visiwa vya Solomon | Tonga | Tuvalu | Vanuatu | Wallis na Futuna |
Makala hii kuhusu eneo fulani bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu eneo hilo kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Je, unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.
|