Claudine André
Claudine André ni mwanaharakati wa uhifadhi wa maliasili wa Ubelgiji. Alizaliwa huko La Hestre,tarehe 6 Novemba 1946. Alianzisha hifadhi inayoitwa Lola ya bonobo mnamo mwaka 1994, ambayo ni hifadhi maalumu kwa ajili ya jamii ya nyani wanaojulikana kama bonobo huko kusini mwa Kinshasa, Mont Ngafula, katika Bonde la Lukaya, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo . [1]
Madhumuni ya hifadhi hiyo maalumu ni kukusanya bonobo wachanga, wengi wao wakiwa yatima kutokana na vitendo vya wawindaji haramu, na hatimaye kuwarudisha katika hifadhi ya msitu. Katika mwaka huo huo, Claudine André alianzisha kikundi cha Marafiki wa Wanyama nchini Kongo, ambako bado ni raisi.
Marejeo
hariri- ↑ "The story of Lola ya Bonobo". Lola ya Bonobo. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 5 Juni 2008. Iliwekwa mnamo 12 Machi 2011.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link)
Makala hii kuhusu mtu huyo bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Claudine André kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |