Coco (filamu ya 2017)
filamu ya 2017
(Elekezwa kutoka Coco (2017 film))
Coco ni filamu ya kufurahisha ya vibonzo (katuni) iliyotengenezwa Marekani mnamo mwaka 2017 na kompyuta za Pixar Animation Studios na kusambazwa na Walt Disney Pictures.
Filamu hii imeundwa kulingana na mawazo ya Lee Unkrich huku akiwa kama Mkurugenzi pamoja na mkurugenzi wake msaidizi aitwaye Adrian Molina. Katika filamu hiyo walioingiza sauti ni Anthony Gonzalez, Gael García Bernal, Benjamin Bratt, Alanna Ubach, Renée Victor, Ana Ofelia Murguía pamoja na Edward James Olmos.
Filamu hii inamuhusu kijana wa kiume wa miaka 12 aitwaye Miguel ambaye anapelekwa katika ardhi ya wafu kwa bahati mbaya. Huko anamtafuta babu yake ambaye anampa msaada wa kurudi katika maisha ya watu waishio na kwenda kuvunja mwiko wa Muziki katika familia yao.
Makala hii kuhusu filamu fulani bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Coco (filamu ya 2017) kama waigizaji wake, hadithi au matoleo yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |