Familia (kutoka Kilatini "familia") ni kikundi cha watu wanaokaa pamoja kama baba, mama na watoto. Kikundi hicho mara yingi ni sehemu ya kundi kubwa zaidi la ukoo unaounganisha watu wenye asili katika uzazi wa pamoja.

Familia pana ya baba, mama, watoto na ndugu wengine, Basankusu, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.
Familia pana ya machotara huko Cape Town, Afrika Kusini.
Sanamu ya Familia: wazazi na mtoto.
Mama na watoto, Berlin, Ujerumani, 1962.
Baba na watoto, Kopperston, Marekani, 1946.

Aina za familia hariri

Aina za familia zinatofautiana duniani kutokana na utamaduni na hali ya jamii.

Katika nchi nyingi za Afrika familia ndogo ya baba, mama na watoto kwa kawaida ni sehemu tu ya familia kubwa zaidi pamoja na ndugu wa baba na mama, akina babu na bibi na kadhalika. Lakini hata Afrika kuna taratibu tofautitofauti kama ni ndugu wa baba au ndugu wa mama wanaotazamiwa kuwa karibu zaidi kwa watoto wa familia ndogo.

Vilevile kuna tofauti kama muundo wa kawaida ni mume mmoja na wake wengi na kila mmoja akiwa na watoto wake tena.

Katika jamii za nchi zilizopita kwenye mapinduzi ya viwandani kama Ulaya na Marekani familia inamaanisha hasa familia ndogo inayokaa pamoja katika nyumba. Ukoo haujapotea lakini umuhimu wake umepungua sana na mara nyingi ni chaguo la watu ndani ya ukoo kama wanapenda kujumuiana na ndugu zao au la.

Katika mazingira ya miji mikubwa au pale ambako koo za kale zimeporomoka na kuachana kuna jumuiya ndogo sana kama mama na watoto ambao ni familia bila baba au wanaume. Aina hii ya familia yenye mzazi mmoja tu imepatikana pia kama familia ya baba na watoto kama utamaduni unamruhusu baba peke yake kulea watoto.

Katika mazingira ya umaskini, vita au mabadiliko ya haraka sana kuna pia watoto wengi wanaoishi kwa bibi au babu na hata hali hii ni aina ya familia.

Viungo vya nje hariri

 
Wikimedia Commons ina media kuhusu:
  Makala hii kuhusu mambo ya utamaduni bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Familia kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.