Come On Over
"Come on Over" ni wimbo ulioshinda katika Grammy Awardambao umeimbwa na mwimbaji kutoka Canada Shania Twain. Ilikuwa Single ya tisa kwa country adio na pia iliipa jia albamu yake ya 1999 Come on Over. Ulitungwa na Twain na aliyekuwa mumewe wakati huo, Mutt Lange. Ilitolewa mara ya kwanza kwa redio za Country za Amerika Kaskazini mwishoni mwa 1999. Wimbo huu ulinawili hadi kushinda tuzo la Grammy mnamo 2000.[1]. Baadaye wimbo huu ulishirikishwa katika albamu ya 2004 ya Twain Greatest Hits
“Come on Over” | ||
---|---|---|
Single ya Shania Twain | ||
B-side | "Man! I Feel Like a Woman!" |
Upokelezi wake
haririBillboard magazine ilipokea wimbo huu kwa kuusifu huku wakiutaja kama ujumbe wa kuchangamsha uliotozwa ndani ya Muziki na wakngamua kuwa ungekuwa hit kwa siku zijazo[2]
Video
haririKanda ya Video ya Muziki kwa "Come on Over" ilichukuliwa kutoka katika DVD ya live ya 1999 ya Twain katika tamasha jijini Dallas. Ilitayarishwa mnamo 12 Septemba 1998 na kutolewa zaidi a mwaka mmoja baadaye mnamo 6 Oktoba 1999. Inaelekezwa na Larry Jordan. Hii ni video ya pili ya ‘’live’’ iliyotolewa kutoka albamu ya Come on Over kufuatia "Honey, I'm Home". Video iliyofuatia baada ya "Come on Over" ilikuwa "Rock This Country!" ambayo ilitolewa katika tamasha. Video hii inapatikana katika DVD ya Twain ya The Platinum Collection.
Unawili Katika Chati
hariri"Come on Over" iliingia katika chati ya Billboard Hot Country Singles & Tracks katika juma la 11 Septemba 1999 katika nafasi ya 52, Debut ya juu kabisa ya juma. Single hii ilikaa kwa chati kwa majuma 20 na ikapanda hadi kufikia #6 mnamo Mesemba 4, 1999, ambapo ilikaa kwa majuma mawili. "Come on Over" ilikuwa single ya nane katika kumi bora kutoka albamu ya Come on Over, single yake ya 12 kwa ujumla, na pia ya 15 katika single ishirini za juu. Katika Billboard Hot 100, ilifikia kilele katika nafasi ya 58 ingawa ilifika #43 katika chati ya Hot 100 Airplay. Nchini Canada, wimbo huu ulianzia #1 katika chati ya RPM Country Singles.[3].
Matoleo Rasmi
hariri- Albamu ya Asili (2:55)
- Toleo la Kimataifa (2:55)
- Live from Dallas (3:00)
Chati
haririChati[4] | Kilele |
---|---|
Canadian Singles Chart | 19 |
Canada RPM Country Singles | 1 |
U.S. Billboard Hot Country Singles & Tracks | 6 |
U.S. Billboard Hot 100 | 58 |
Vidokezo
hariri- ↑ http://www.shaniatwain.com/about-awards.asp Archived 19 Julai 2009 at the Wayback Machine. Shania Twain awards
- ↑ Billboard, 11 Septemba 1999
- ↑ "RPM Volume 70 No. 2, November 01, 1999". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2012-03-09. Iliwekwa mnamo 2010-01-21.
- ↑ https://web.archive.org/web/20060317013239/http://www.billboard.com/bbcom/retrieve_chart_history.do?model.vnuArtistId=34388&model.vnuAlbumId=562635 Billboard chart history
Alitanguliwa na "Something Like That" ya Tim McGraw |
RPM Country Tracks Single inayoongoza 1 Novemba-8 Novemba 1999 |
Akafuatiwa na "I Love You" by Martina McBride |