Shania Twain (jina la kiraia: Eilleen Regina Edwards; amezaliwa 28 Agosti, 1965) ni mtunzi wa nyimbo na mwimbaji kutoka nchini Kanada. Kwa karibu miaka 25 akiwa katika tasnia ya muziki, Twain ameuza zaidi ya rekodi milioni 85 na msanii aliyeuza vyema katika historia ya muziki wa country kwa upande wa wanawake.[2] Mafanikio yake yamempatia heshima kubwa na kupewa cheo cha "Malkia wa Country Pop".[3]

Shania Twain
Twain katika Canadian Music Hall of Fame akiwekewa nyota, 2011
AmezaliwaEilleen Regina Edwards
28 Agosti 1965 (1965-08-28) (umri 58)
UtaifaMkanada
Kazi yake
Ndoa
  • Robert John "Mutt" Lange (m. 1993–2010) «start: (1993)–end+1: (2011)»"Marriage: Robert John "Mutt" Lange to Shania Twain" Location: (linkback://sw.wikipedia.org/wiki/Shania_Twain)
  • Frédéric Thiébaud (m. 2011–present) «start: (2011)»"Marriage: Frédéric Thiébaud to Shania Twain" Location: (linkback://sw.wikipedia.org/wiki/Shania_Twain)[1]
Watoto1 Musical career
Ala
Miaka ya kazi1973–hadi sasa
StudioMercury Nashville
Wavutishaniatwain.com

Albamu ya pili ya Twain, ya mwaka wa 1995 The Woman in Me, imemletea mafanikio makubwa kwa kuuza nakala milioni 20 dunia nzima, ikiwa na vibao vikali kama vile "Any Man of Mine" kilichompatia Grammy Award. Albamu ya tatu ya Twain, Come On Over, imekuwa albamu iliyouza vyema kwa muda wote kwa upande wa wasanii wa kike katika miondoko ya albamu za country kwa muda wote, imeuza kwenye nakala milioni 40 dunia nzima.[4]

Come On Over imezalisha vibao vikali kadhaa, ikiwa ni pamoja na "You're Still the One", "From This Moment On" na "Man! I Feel Like a Woman!", na kumpatia Twain Grammy Awards nne. Albamu yake ya nne Up!, ilitolewa mnamo mwaka wa 2002 na, kama jinsi ilivyokuwa katika albamu zake mbili zilizopita, nazo zilitunukiwa Diamond nchini Marekani, vibao vyake vikali ni pamoja na "I'm Gonna Getcha Good!" na "Forever and for Always".

Twain amepokea Grammy Award tano, tuzo za BMI Songwriter 27, nyota kadhaa kwenye Canada's Walk of Fame na Hollywood Walk of Fame, na vilevile katika Canadian Music Hall of Fame.[5] Ni msanii wa kike pekee katika historia kuwa na albamu tatu mfululizo zilizotunukiwa Diamond na RIAA.

Pamoja na yote, Twain yupo nafasi ya 10 kwenye zama za wasanii bora za Nielsen SoundScan.[6]

Mwaka wa 2004, Twain amestaafu kuimba na kurudi nyumbani kwao huko nchini Switzerland.[7] Katika tawasifu yake mwaka wa 2011, ametaja ya kwamba udhaifu wa sauti yake umepelekea kuacha kuimba katika hadhara.[8]

Wakati vyote kuimba na kuongea kwake kulivyoathirika, Twain alielekea kupata ushauri wa kitiba katika Kituo cha Vanderbilt Dayani huko mjini Nashville. Wataalamuo hao wamekutana na tatizo fulani katika sauti yake, yote yanatibika huku kukitakiwa uangalifu na utulivu wa nguvu wakati wa matibabu.[9]

Mwaka wa 2012, Twain amerejea tamashani na akiwa na onesho lake kabambe la Still the One, lililofanyika katika kumbi ya The Colosseum at Caesars Palace. Mwaka wa 2015, Twain amerejea barabarani kwa kile alichokiita ziara yake ya kuagana. Ziara iliitwa Rock This Country iliyoanza mnamo Juni 5, 2015 mjini Seattle, Washington na kuenda hadi Oktoba 27, 2015 huko mjini Kelowna, British Columbia, Canada.[10]

Diskografia hariri

Tanbihi hariri

  1. Billups, Andrea. "Shania Twain Announces Farewell Tour in North America". People.com. Iliwekwa mnamo March 5, 2015.  Check date values in: |accessdate= (help)
  2. "CAS – Central Authentication Service". Oxfordmusiconline.com.ezproxy2.library.arizona.edu. Iliwekwa mnamo March 5, 2015.  Check date values in: |accessdate= (help)
  3. Gordinier, Jeff. "Shania Twain Does Not Believe In Tears | News", EW.com, November 8, 2002. Retrieved on March 4, 2011. Archived from the original on 2011-09-25. 
  4. Twain, Shania, Atria Books Inks Deal for Shania Twain Memoir, Shania Twain website, ilihifadhi kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2010-12-20, iliwekwa mnamo January 19, 2011  Check date values in: |accessdate= (help)
  5. "Shania's Awards". Ilihifadhi kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2014-09-07. Iliwekwa mnamo 2016-08-10. 
  6. BLABBERMOUTH.NET — METALLICA Among Top-Selling Artists Of SOUNDSCAN Era, Roadrunnerrecords.com, iliwekwa mnamo October 1, 2009  Check date values in: |accessdate= (help)
  7. "NASHVILLE SKYLINE: Shania Twain Heads to Las Vegas: Is it the Promised Land or the Elephants’ Graveyard?". CMT. Iliwekwa mnamo March 5, 2015.  Check date values in: |accessdate= (help)
  8. "Shania Twain Not Only Lost Husband, But Also Voice". Billboard. Iliwekwa mnamo March 5, 2015.  Check date values in: |accessdate= (help)
  9. "Nashville clinic saves voices of the stars", USA Today, October 31, 2011. Retrieved on July 21, 2015. 
  10. "http://news.shaniatwain.com/". news.shaniatwain.com. Ilihifadhi kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2016-08-23. Iliwekwa mnamo October 9, 2015.  Check date values in: |accessdate= (help)

Vyanzo hariri

Viungo vya nje hariri