Mtandao wa kompyuta ni mpangilio wa kompyuta zenye kubadilishana rasilimali zinazopatikana au kutolewa kwenye fundo za mtandaoni. Kompyuta hutumia itifaki zinazofahamika kwa mawasiliano kwenye muingiliano wa kidijitali kuwasiliana zenyewe kwa zenyewe.Huu muingiliano umetengenezwa na teknolojia ya mtandao wa Mawasiliano ya simu kwa msingi wa mbinu za kutumia waya, vifaa vya macho na mawimbi ya redio ya bila waya ambazo zinaweza kupangiliwa katika itifaki mbalimbali za mtandao.

Pindo za mtandao wa kompyuta huweza kujumuisha kompyuta ya mtu binafsi, seva, mtandao wa vifaa vigumu, au vitu vingine maalumu au vitu vyenye lengo kuu. Huweza kutambulika kwa anwani ya mtandao na pia huweza kuwa na majina la kifaa husika. Majina ya kifaa husika husaidia kama kumbukumbu inayowekwa katika pindo na mara chache hubadilika baada ya utambulisho wa mara ya kwanza. Anwani ya mtandao husaidia kwa kuonyesha na kutambulisha pindo kwa itifaki ya mawasiliano kama vile itifaki ya mtandao.

Historia hariri

Mtandao wa kompyuta huweza kuchukuliwa kama tawi la sayansi ya kompyuta, uhandisi wa kompyuta na mawasiliano ya simu, kwa sababu huegamia katika programu tumizi ya nadharia na kwa vitendo ya mambo yanayoendana. Mtandao wa kompyuta uliwezeshwa na maendeleo na historia ya technolojia kubwa ya safu.

  • Mwaka 1950, mtandao wa kumpyuta ulitengenezwa na shirika la kijeshi la U.S. Semi-Automatic Ground Environment (SAGE) lenye mfumo wa rada wa kutumia kengele 101 za kifaa cha kimtandao kinachobadilisha ishara za mawimbi. Ilikuwa ni kifaa cha kimtandao cha kwanza cha kibiashara kilichotolewa na ushirikiano wa AT&T mwaka 1958. Hicho kifaa kiliruhusu taarifa kusafirishwa katika njia za simu zisizo na mazingira halali katika spidi ya biti 110 kwa kila sekunde.

Matumizi hariri

Mtandao wa kompyuta umepanua mawasiliano ya watu kwa njia za kielektroniki kwa teknolojia mbalimbali kama email, ujumbe wa papo hapo, mawasiliano ya ndani ya mtandao, kupiga simu za sauti na video pamoja na mikutano ya video. mtandao umeruhusu kuhusiana kwa rasilimali za kompyuta na mtandaoni. Watumiaji wanaweza kupata na kutumia rasilimali zinazotolewa kwenye mtandao, kama vile utoaji wa mfanano wa picha au kutumia sehemu moja inayohifadhi taarifa. Mtandao umeruhusu kushiriki katika mafaili, taarifa na aina zingine za taarifa kuwapa watumiaji wanaoruhusiwa uwezo wa kupata taarifa zilizohifadhiwa kwenye kompyuta nyingine kwenye mtandao. Mgawanyiko wa kikompyuta hutumia rasilimali zilizopo kwenye mtandao kukamilisha kazi zake.