Wikipedia:Mwongozo (Kutaja vyanzo)

Utangulizi   Kuhariri   Kuanzisha Makala   Muundo   Viungo vya Wikipedia   Kutaja vyanzo   Kurasa za majadiliano   Kumbuka   Kujisajili    

Vyanzo vya habari ni mahali tunapopata habari zetu za hakika. Katika wikipedia vyanzo hivi vinatakiwa kuonekana maana habari zisizo na vyanzo kuna uwezekano mkubwa wa kuondolewa.

Katika wikipedia yetu mara nyingi si rahisi kuonyesha vyanzo kwa sababu wachangiaji wengi hawana nafasi ya kutumia maktaba mazuri penye majarida na vitabu vya kitaalamu.

Kwa hiyo tutatumia mara nyingi vyanzo visivyo vya Kiswahili hasa Kiingereza. Ni sawa kunakili orodha ya vyanzo kutoka makala ya en:wikipedia. Kuna pia vyanzo vizuri vinavyopatikana mtandaoni.

Tanbihi chini ya ukurasa

Njia nyepesi kuonyesha chanzo cha habari ni tanbihi (footnotes) chini ya ukurasa. Hapa kuna alama Marejeo.jpg kwenye menyu ya kuhariri chanzo.

Ukibofya hapa unapata dirisha la Wikipedia-menyu-ingiza marejeo.png.
Sasa andika chanzo au maelezo mengine katika nafasi yake chini ya maneno "Maandishi ya marejeo".

Bado hatua moja: chini ya makala mwishoni kabla ya interwiki andika:

===Marejeo===

<references/> AU {{marejo}} na vyanzo ulivyotaja kwenye mabano au maelezo vitaorodheshwa hapo.


Kama chanzo chako ni tovuti ya intaneti (nje ya wikipedia) fanya hivyo:

  • weka kiungo cha nje kwa kuandika mabano mraba [ ] - mara moja tu, si mara mbili jinsi ilivyo kwa viungo kwa makala mengine ya wikipedia!. Kati ya mabano haya unaingiza anwani ya intaneti (unaweza kutaipu pia)
[http://www.example.com] jina la kiungo
  • andika anwani ya tovuti kati ya mabano mraba, acha nafasi tupu 1,2 kabla ya mabano ya pili halafu ongeza maneno ya maelezo
[http://www.example.com Maelezo yanayoonekana]

Usitaje makala mengine ya wikipedia kama chanzo lakini unaweza kunakili vyanzo kutoka huko KAMA VINAFAA.

Viungo vya Nje

Makala mengi ya wikipedia huwa na sehemu mwishoni inayoitwa "Viungo vya Nje".

Hapa tunaweka viungo vya Nje kwa tovuti zenye maana na kukubalika zinazohusu kichwa na yaliyomo ya makala..

Inatosha kutaipi anwani kamili ya tovuti unayotaka kurejea:

http://www.britannica.com/EBchecked/topic/336408/Leonardo-da-Vinci


Jaribu ulichojifunza katika sanduku la mchanga

Endelea kufunzi na Kurasa za majadiliano

Namna ya kutaja vyanzo

  • Kutaja marejeo katika kitabu: Utataja jina la mwandishi, jina la kitabu, mwaka wa kuchapishwa na mahali pake, kampuni ya kuchapisha, ukurasa au kurasa penye habari unazorejelea
  • Kutaja marejeo katika gazeti au jarida: utataja jina la mwandishi (kama lipo), kichwa cha makala, jina la gazeti/Jarida, tarehe yake
  • Kutaja marejeo kutoka intaneti: utataja jina la mwandishi (kama lipo), kichwa cha makala, jina la tovuti, tarehe yake, unaongeza tarehe ulipoangalia tovuti, URL (=anwani ya intaneti). Huwezi kutumia tovuti yoyote. Facebook, twitter na "social media" kwa jumla si vyanzo vinavyofaa kuunda umaarufu au umuhimu wa habari.