Cosmo Gordon Lang
William Cosmo Gordon Lang, 1st Baron Lang of Lambeth, GCVO, GCStJ, PC (alizaliwa 31 Oktoba 1864 – 5 Desemba 1945) alikuwa kasisi wa Kianglikana kutoka Uskochi ambaye alihudumu kama Askofu Mkuu wa York (1908–1928) na Askofu Mkuu wa Canterbury (1928–1942). Uteuzi wake kuwa Askofu Mkuu wa York, miaka 18 tu baada ya kuwekwa wakfu, ulikuwa wa haraka zaidi katika historia ya kisasa ya Kanisa la Uingereza. Kama Askofu Mkuu wa Canterbury wakati wa mgogoro wa kujiuzulu kwa mfalme mwaka wa 1936, alichukua msimamo mkali wa maadili; maoni yake katika matangazo ya baadae yalilaaniwa sana kwa kuonekana kuwa hayakuwa ya huruma kwa mfalme aliyejiuzulu.[1]
Marejeo
hariri- ↑ McCraw, Ian (2000). The Kirks of Dundee Presbytery. Dundee: Friends of Dundee City Archives. uk. 46. ISBN 0-9536553-2-6.
Makala hii bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari. |